Thursday, December 23, 2010

Maisha ni jinsi mtu unavyojipanga.
Kipendezacho machoni pako, ni kwa jinsi unavyokiona wewe mwenyewe, kwani mwingine kinaweza kuwa kinamuudhi, japo wewe wakipenda sana.

Kila kitu kwa mfano wake waweza kukifanya kikafanana na akili yako inavyotaka, na ndio maana hao ndege watatu warukao angani katika picha hii, unaweza kufananisha na kitu fulani unachokifahamu, au unachotaka kiwe.

Kwa ufupi nataka kuwaasa kuwa maisha ni chaguo lako mwenyewe, furaha itakuwepo, iwapo utakubali hali uliyonayo na kujaribu kuitunza kama ilivyo au kuiboresha mwenyewe.

Tunapoelekea kuanza mwaka mpya wa 2011, basi tuzingatie hayo.

Merry Christmas and Happy New Year 2011!
Photo from Oman Collective Intelligence

Thursday, December 16, 2010

Thought of the Day

You can study and get any certificates. But you cannot get your death certificate

You can become an engineer if you study in engineering college. But you cannot become a president if you study in Presidency College

You can expect a BUS from a BUS stop ... But you cannot expect a FULL from FULL stop

A mechanical engineer can become a mechanic but a software engineer cannot become a soft

You can find tea in a teacup. But you cannot find world in the world cup

You can find keys in Keyboard but you cannot find mother in the motherboard

Lastly, can the great abdominal surgeon perform same surgery to his/her abdomen??!!!

Friday, December 10, 2010

Weekend Irish Quotes!

A good laugh and a long sleep are the two best cures

Who gossips with you will gossip of you

For every wound, a balm.
For every sorrow, cheer.
For every storm, a calm.
For every thirst, a beer!

Again......Wishes you a lovely weekend!

Cheers!

Friday, December 3, 2010

Nani zaidi?

I am not sure if this is competititon or just natural phenomena..

I wish you a cheerful weekend! And, you can guess what is going up there.

Wednesday, December 1, 2010

Upinzani Tanzania Maana Yake ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe

Upinzani Tanzania, unaelekea kupoteza uelekeo kwa sasa.

Ule msingi wa upinzani kufanya juhudi ya kuiangalia na kuikosoa serikali (watch dog) sasa ujaelekea kupata doa.

CHADEMA ambacho ni chama kilichokuwa kinatarajiwa na wengi kuonyesha cheche za moto, badala ya kujipanga kutetea maslahi ya nchi, kimeanza kugeuka na kuanza kuwashiana moto ati kwa nini watu hawakwenda bungeni na kudai ni watoro, kwa hiyo wajieleze kimaandishi.

Mimi naona ni ubabe usio na maana sana, nafikiri ulikuwa ni wakati wa CHADEMA kushikamana na kupanga mikakati ya kuleta maendeleo kuliko kuanza kunyoosheana vidole.

Hii inatupa picha mbaya kama kitaingia madarakani, kwani kinaelekea kuwa chama cha migogoro na vurugu.

Kina wajibu wa kutulizana kuliko kuleta mkanganyiko na mwishowe kuporiomoka kama NCCR mageuzi ilivyoporomoka wakati uleee wa Mrema vs Marando.

Jameni, mtusaidie nyieeee

Thursday, November 25, 2010

Mtazamo wangu Katika Baraza Jipya la Mawaziri 2010

JK ametangaza baraza jipya la mawaziri.
Lina sura nyingi mpya, na watu wengi kama sio wote, hawajawahi kuhusishwa na tuhuma nzito au ufisadi.

Kuna mmoja au wawili, nyendo zao kimahusiano na wengine hazikuwa nzuri sana, na walikuwa ni watu wakati mwingine wa kuropoka na kudandia vitu, na hata kuwakejeli wafanya biashara maarufu walio safi.

Watu watahoji kwa nini JK ameweka wanawake wachache kuliko watu walivyotumainia?

Mimi kwangu hainikuni kichwa, kwani aliahidi kuweka watu wenye ufanisi, watakaondoa ukiritimba, wachapa kazi na walio karibu na wananchi wote wa Tanzania. Kwa maana nyingine maslahi ya Taifa mbele.

Dhana ya kuchagua wanawake tu mradi kufurahisha kundi la watu fulani hatupaswi kuliweka mbele, tunapenda pale ambapo mwanamke ana sifa sawa na mwanaume, basi hapo ndipo mwanamke atakapopendelewa, na sio hata yule aliye hoi na mbumbumbu wa kitu fulani basi na apewe nafasi ya uongozi eti kwa sababu tu ni mwanamke. Mambo yote haya yapo sambamba na kupiga vitu undugunaizesheni katika kazi.

Kama una rafiki au ndugu ambaye ni mchapa kazi na mwadilifu, kwa nini asipewe nafasi wakati sifa zote anazo. Mimi ninaamini ukiwa muadilifu, basi unatafuta na marafiki waadilifu, ukipata nafasi ya kuchagua wachapa kazi, basi kama rafiki yako ana uwezo naye anapewa nafasi. Kama ni goigoi, basi hana nafasi. Na hakuna atakayekulaumu kwa kumtupilia mbali.

Napenda wanawake tuchukue hii changamoto kwa hali ya uchanya, tusihoji kwa nini wanawake ni wachache, bali kwa nini tusijitahidi na sisi kupata nafasi hizo. Nina imani tunaweza kama tutajiamini na kuongeza bidii. Tusisubiri kila kitu kuamuliwa, halafu tunaenda kulalama pembeni bila kuongeza juhudi.

Sina budi kutoa pongezi hasa kwa baadhi ya mawaziri wanawake kama Prof Tibaijuka, Mama Kombani, Mary Nagu na wengineo huku nikiendelea kusubiri matunda ya baraza jipya la mawaziri kama kweli litatoa dira ya uelekeo wa CCM kwa miaka mingine 5, kwani kwa muda uliopita, tulitiwa kichefuchefu, tuna matumaini hatutatapishwa sasa.

God bless Tanzania

Friday, November 19, 2010

Kampeni za Uchaguzi 2015 Kumbe Zimesha Anza

Wakati watu wengine wanahangaika na kuona CHADEMA kitafanya nini kwenye bunge lijalo, kumbe kuna baadhi ya waheshimiwa wamekwisha anza kujipanga kwa ajili ya kugombea urais 2015.

Habari hizi ambazo bado zipo kwenye mvumo wa kichini chini zinadai kuna wanasiasa maarufu na wenye majina makubwa ambao wameshawahi kuwa mawaziri wameanza mkakati mkubwa wa kuhakikisha wanachaguliwa kuwa viongozi wa nchi.

Kati yao wapo waliowahi kuwa mawaziri na wakalazimika kujiuzuru nyadhifa zao kufuatia kashfa zilizowaandama ndani na nje ya bunge.

Yasemekana pia kuna aliyewahi kuwa waziri mkuu, na anaonekana amepania vilivyo, kwani alianza kampeni mapema hata kabla ya uchaguzi wa 2010 kufanyika. Na amekuwa hataki kujionyesha ya kuwa anawania kiti hicho, lakini ameshaunda kamati yake ya ushindi! Na anaendelea "kununua" watu ili wamuunge mkono wakati ukiwadia.
Habari hii inaweza kuwa uzushi, lakini mara nyingi kwa siasa zetu hizi chafu na safi, chochote kinawezekana.

Kwa mtazamo wetu, tunahisi wale wenye kashfa ambazo hazijafutika au kuamuliwa kihaki, wana nafasi ndogo ya kupenya ili wawanie uongozi hasa wa nchi kwa siku zijazo.

Tukumbuke kuchagua mbivu na si mbichi au pumba

Thursday, November 11, 2010

Uchaguzi wa Spika Tanzania... Ni Ujanja tu au?....

Inaelekea kuwa vurugu, mipasuko na vidonda vya uchaguzi bado havijapona!!

Suala la msukumo wa kumpata spika wa Bunge la Tanzania unaingia sura mpya mara baada ya CCM kuwachagua wanawake tu kushindanishwa,

Binafsi, nalipongeza suala hili, kwani inaonekana kama vile inajali wanawake, lakini unaweza kukuta ukweli ni kuwa wameona hao mafahali waliokuwa wanatonyana kwenye vyombo vya habari hawawezi kukaa zizi moja iwapo mmoja watampa nafasi ya kukaa juu ya mwingione, ndio maana wakateua wananwake tu! Kama misingi ilikuwa ni ya mtazamo huu, basi bado CCM hawakuwa na mpango wa kuteua wanawake, isipokuwa kuwageuza jamvi la kuficha uovu wao kwa kuwaendesha kwa remote :-(

Kuna wengine waliopendekezwa tulishawasahau kwenye nyanja za siasa... lakini mara wameibuka katika kugombea uspika....sasa hapo kweli sio kwamba wamepanga kwa makusudi mtu fulani kwa matakwa yao?

Saturday, November 6, 2010

Kikwete Aapishwa Kuwa Rais 2010 - 2015

HAYA. Mambo yanaelekea yamekwisha, leo JK ameapishwa baada ya kuchaguliwa na 27% ya watanzania waliojiandikisha kupiga kura, na 61% ya wale waliojitokeza kupiga kura!

Hapo hakuna cha kujivunia, ila kushukuru Mungu tu kuwa labda wale ambao hawakujitokeza wangepigia upinzani!

Nawapa pole wanafunzi wote wa vyuo, kwani hawakuweza kupiga kura baada ya serikali kuamua vyuo visifunguliwa hadi uchaguzi uishe ilhali wanafunzi wengi walijiandikisha wakati wakiwa chuoni. Nina hakika wengi walikuwa wanataka mabadiliko.

Ndio mwanzo huu, tunasubiri sasa mambo ya kukata rufaa na muda wa kuanza serikali mpya, tukiwa na matumaini kutakuwa na mabadiliko makubwa kiutendaji, na baadhi ya watu kupoteza ubunge wao kupitia mahakama.

Picha kutoka michuzi

Friday, October 29, 2010

Wimbo wa Uchaguzi kwa Sasa

Lala salama hiyooooo
Uchaguzi unakaribia
Vijana tupo tayari kuleta mapinduzi
Tumejiandikisha
Ni lazima tupige kura na kuweka historia
Wazee wote wang'oke
Mafisadi hawana nafasi
Tunataka maendeleo kwenda mbele na si vinginevyo
Mgombea wangu kura yangu anayo

Je na wewe mgombea wako unamuahidi nini?

Tafadhali jitokeze kupiga kura yako siku ya jumapili.

Tutashinda tu!

Monday, September 27, 2010

Ahadi Za Kampeni za Kisiasa TZ Zimepakwa Rangi tu

Kwa nyie mnaosikiliza kampeni za uchaguzi....

Hivi mmekwisha tafakari wenzetu wanayoahidi?

Kila mtu anaimba wimbo wake, sina hakika kama kila mtu atatimiza hayo kwenye miaka mitano anayo omba tumpe kura zetu ati atuwakilishe.

Mimi nitajenga uwanja wa ndege wa kimataifa katika kila wilaya!!!!

Mimi nitatoa elimu ya bure tangu mtoto akiwa tumboni kwa mama yake mpaka atakapo ng'oka jino la mwisho la uzeeni!!!

Mimi nitajenga meli mpya kila mto hapa Bongo, ili watu wasiliwe na mamba tena!!!!

Mimi nitahakikisha kwa muda wa wiki 2 tu, jimbo langu lote litakuwa na maji ya uhakika kwa mwaka mzima na barabara zinazopitika kila siku. (Hapo nina maana ya waenda kwa miguu, na maji ya uhakika mvua zitakapokuwa zinanyesha)

Mimi nitatoa ajira kwa watu wote, ukipata ujauzito, njoo umwandikishie mtoto wako kazi kabisa, ili akizaliwa anaanza ajira rasmi moja kwa moja...

Mimi nitatokomeza ufisadi na kilimo cha bangi kila mahali hata ikulu kama inalimwa huko!!!!!

Huo ndio mwelekeo wa kampeni, kama unatafakari, utang'amua yote, kwa jinsi ambavyo umeona mifano yangu, basi jua mwananchi wa kawaida ndio anaelezwa ahadi za namna hii.

Monday, September 20, 2010

No No .. to Sex

Electric fence! Ha ha haaaa

Wednesday, September 15, 2010

Uchaguzi Tanzania:Maswali maswaliii

Kwa haraka haraka

Nimekuwa nikfuatilia kampeni za siasa, kwani sitaki kufanya makosa wakati utakapowadia wa kumchagua kiongozi wangu wa baadaye, ukizingatia ya kuwa hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika zoezi zima la kupiga kura za kuchagua viongozi wa nci yetu,

Nimekuwa nikisikiliza kwa makini sera za wagombea mbalimbali na kuzipima kama zina ukweli, ushawishi, na pia kuangalia kama kweli zinatekelezeka au ni changa la macho.

Nahisi naanza kukata tamaa, kwani wanasiasa au wagombea nafasi za kisiasa badala ya kuhubiri sera za vyama vyao, wamekuwa mstari wa mbele kusikiliza mwenzie alisema nini, na wao kusema ya kwao kutokana na wengine walichosema hapo awali, na mwisho hakuna kampeni tena bali ni kupeana vidonge na kujibu mapigo!!!!!

Sie tunaotaka kupima sera tumejikuta tukipima nani ni bingwa wa kujibu mashambulizi, na mara ,,, hatimaye zoezi la kupiga kura litafika.. sasa hapo tutampigia kura nani?, nahisi hatutakuwa tumempata kiongozi atakayekidhi tulichotaka kusikia kabla ya kuamua.

Mpaka sasa mimi naona wengi ni wahuni na matapeli tu. Wanabembeleza wachaguliwe kwa matakwa yao binafsi. Na kwa maono yangu, naona vyama vimeelekeza nguvu na pesa nyingi kwa wagombea urais, kwani kutumia helikopta nyingi na magari utitiri kwa mgombea mmoja, wakati wagombea ubunge na udiwani wakiswaga lami ni kuonyesha ishara ya uchoyo na unafiki tu

HATUDANGANYIKIIIIIII

Thursday, September 9, 2010

Friday, September 3, 2010

Have a Blessed Weekend


All the blessings of Mother Theresa and Pope John Paul II has been showered to you my reader.
See you next time!!

Tuesday, August 31, 2010

Maadili ya Uchaguzi Tanzania ni Yapi?

Huu ni msimu wa kisiasa Tanzania

Ni vigumu kufunga midomo kuzungumzia siasa hata kama hupendelei mambo ya siasa.


Kuna kitu ambacho sikielewi kuhusu sheria mpya ya matumizi ya fedha katika uchaguzi wa Tanzania, hasa pale wanapozungumzia matumizi ya lugha au kwa kifupi kufuata maadili.


Inaonekana kuna baadhi ya vyama wakihusishwa na tuhuma fulani za ufisadi, hata kama tuhuma hizo hizi zilisababisha watu katika chama hicho kujiuzulu na wengine kushitakiwa, kwa sasa wanakuja juu.


Kwa anaye elewa hayo maadili, naomba anielimishe!!

Tuesday, August 24, 2010

Ni Ukweli Huu

Lazima tukubali.

Tunavuna tulichopanda, na tunakula kile tunachokifikia.
Kama hufikii vilivyo nona, kuna sharti lazima ulitimize... Maana yake, ni lazima uhangaike.

Nawatakia siku njema

Tuesday, August 17, 2010

Uteuzi wa Baadhi ya Wagombea Wabunge CCM ni Utata Mtupu

Uteuzi wa majina ya wagombea ubunge kwa CCM umekuja kwa hisia tofauti hasa baada ya baadhi ya wagombea walioshinda kura za maoni kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.
Mwakalebela ameenguliwa ati kwa sababu kakiuka maadili, yaani anatuhumiwa kwa rushwa, wakati Mramba na Chenge wana kesi mahakamani, lakini ati wanadai kuwa hawa ni watuhumiwa tu, na kesi haijaamuliwa, kwa hiyo wamepitisha majina yao. Sasa Mwakalebela yeye ameshahukumiwa au ni mtuhumiwa tu?

Mwenye bahati mbaya zaidi ni Hussein Bashe, ambaye alipata kura nyingi sana za maoni jimboni Nzega, lakini ghafla kageuzwa kuwa sio raia wa Tanzania kwa kudai kuwa wazazi wake wote walikuwa wasomali kabla ya kupewa uraia wakati Bashe akiwa na miaka 10.

Kwa sasa Bashe ana umri mkubwa tu, sio miaka 10 na nusu au 11, yaani amekuwa mtanzania mpaka hapo juzi tu ndo ati CCM wanadai sio raia.

Ilikuwaje walimpa nyadhifa mbalimbali huku wakijua sio raia wa Tanzania?
Je asingeshindwa kura za maoni, huo uraia wake ungehojiwa?
Nakumbuka wakati wa uchaguzi wa UVCCM, Bashe alienguliwa tena wakidai umri wake umezidi, wakati hapo awali, viongozi waliokuwepo akiwemo Nchimbi walichaguliwa wakiwa "vijeba".

Je ana bahati mbaya au ni makusudi?

Mimi nahisi CCM wanajua details za wanachama wao, wakiona wewe ni moto wa kuotea mbali, basi fimbo ya kwanza ni uraia. Nakumbuka Jenerali yalimkuta kama haya, Kinana pia.

Kwa nini kusubiri mtu anapoelekea kushinda, ndio mlete stori za kuwa sio raia, wakati ameishi zaidi ya miaka 40 Tanzania, na mmempa mpaka na pasi ya kusafiria na wala hakuna aliyesema kuwa huyu sio mbongo.

Sheria inasema mhamiaji akiishi kinyume cha sheria ya uhamiaji, anakamatwa mara moja na kufunguliwa mashitaka, mbona hapa hatuoni hilo?
Mwajiri wa mtu huyo, naye pia ushitakiwa kwa kosa la kumuajiri raia wa kigeni bila kufuata utaratibu, mbona CCM hawajashitakiwa kwa kosa hilo?

Nafikiri msajiri wa vyama vya siasa anapaswa kuisimamisha CCM ili wanachama wake wachunguzwe uraia :-(

Nafikiri inabidi kufanya uchunguzi wa kina, maana wakati wa mchakato wa kura za maoni, wengi tu walikuwa wanazushiwa ati sio raia wa Tanzania!!!!

Pata njia ya kujua orodha ya wagombea wateule wa CCM hapa

Saturday, August 7, 2010

Uchaguzi wa Rais: Mipaka ya Rwanda Kufungwa?


Rwanda inatarajia kufanya uchaguzi wa Rais wake hapo tarehe 9 agosti 2010.

Kampeni zinasemekana kuwa za amani na hazina vurugu au shughuli nyingi kama ilivyo Kenya, Tanzania na Uganda.

Kuna uwezekano mkubwa Rais wa sasa Paul Kagame akashinda kwa kishindo kama kawaida yake. Uchaguzi uliopita, jimbo la kaskazini walimpa kura za ndiyo kwa asilimia mia moja, yaani watu wote waliopiga kura walimpa kura ya ndiyo. Nafikiri kwa Tz hiyo inahesabika kama ndoto... sasa sijui viongozi wetu sio wasafi au waadilifu?

Habari mpya tunayoisikia, ni kuwa kuanzia Jumatatu mipaka yote itafungwa, hakuna kuingia wala kutoka, sasa sijui ni mpaka lini?

Pia inasemekana ya kuwa wanyarwanda walishapigwa stop kuchukua passport mpya, hasa kwa wale wanaotaka kupata kwa mara ya kwanza miezi kadhaa iliyopita, ati wasubiri mpaka uchaguzi upite!

Hizi habari zinaweza kuwa propaganda au ni za ukweli.


Tunaombea uchaguzi wa amani huko Rwanda.

Monday, August 2, 2010

Kura Za Maoni CCM: Vurugu Tupu

Jamani hizi kura za maoni za CCM mbona zimejaa rafu sana...

Kweli chama hiki ni safi au kimejaa uchafu, yaani madai ya hongo, vurugu, na kila aina ya mambo yasiyo kimaadili katika kuomba ridhaa ya kuwakilisha chama ili kupata viongozi yanasikika.

Cha ajabu na watuhumiwa wa ufisadi, kuna wanaojizolea kura nyingi tu. Tutafika kweli?!!!

Nini mwelekeo wa siasa zetu.


Mimi naogopa kabisa. Itabidi niitumie kura yangu vizuri kumchagua kiongozi wa kweli. Wananchi tusiangushane

Tuesday, July 20, 2010

Siasa: Ni upupu wa Kujipakaa au?

Kampeni za uchaguzi karibu zinaanza...

Mie nauita ni mchezo mchafu, kwani utakuta watu wametulia na ni marafiki na kucheka cheka kila mara.

Ukikaribia uchaguzi watu wana anza kununiana na kuitana majina ya ajabu, sijui mavuvuzela, mara watu wanapandikiziana bangi ili mwenzao akamatwe wapete wao tu kwenye uchaguzi.

Wengine sijui wanaenda Bwagamoyo na kuku wa kijani, mara kuku wa samawati... yooote ya nini hiyo.

Mwisho wakati wa kampeni, ni kupakana matope, kutukanana nk nk, yaani utafikiri ni vichaa fulani hivi.

Kwa nini nisiite ni mchezo mchafu...

Tuesday, July 6, 2010

Monday, June 28, 2010

Likizo na Kombe la Dunia

Jamani hili kombe la dunia naona ni balaa tupu!

Hakuna kinachofanyika, watu kukaa na kukodolea macho runinga na kupiga mayoweeeee.

Mimi nina mapenzi na michezo, lakini michezo hainuchukulii muda wangu wote. Ninasikitika kuona tumeahirisha mitihani ya majaribio eti kwa sababu watu hawataki kukosa kuona kombe la dunia. Hivyo hawawezi kusoma kujiandaa na test!!

Penye wengi, hapakosi neno, na pia wengi wape. Tumepata likizo bila kutarajia....

Tunatumaini kurudia kama kawaida katikati ya mwezi wa julai.

Nawatakia wapenzi wa mpira kipindi chema, kwani sina zaidi la kusema.

Ghana hoyeeee!!!!!

Thursday, June 24, 2010

Williams: Perfect sisters

Happy sisters

Lovely sisters

Champions sisters

Energetic sisters

They love tennis

Wednesday, June 2, 2010

Watanzania Tumerogwa???

Nina maswali mengi sana ninajiuliza kwa nchi yetu ya Tanzania....
Yanakuja haswa pale uchaguzi wa Rais na wabunge unapokaribia.


Kuna kuwa na visa vingi vya watu kushikana uchawi, mara huyu kamroga huyu.
Watu wanapotangaza azma ya kugombea mathalani ubunge, utashangaa aliye na jimbo anaanza kugaagaa na vyombo vya habari, mara apeleke vitisho na kumtaka yule anayetaka kugombea ati ajitoe, au asichukue form ya uchaguzi

Kana kwamba hiyo haitoshi, utaskia vifo vya ajabu na watu wakishikana uchawi.
Lakini si uongo, nasikia wakati huu waganga wa jadi wana soko zuri sana, na ndio wakati wao wa kivuno toka kwa politicians wajinga.
Naogopa kutamka jina la wananchi ambao huwapa wanasiasa wajinga kura, labda wewe msomaji unaweza kuwa na jina zuri.
Jana nilimsikia Pinda akisema hivi watanzania tumerogwa????? Kwa sababu fursa zote tunazo za kujiendeleza, mali ghafi, madini, mito, maziwa, vivutio, amani, viongozi safi na wazuri ( cha ajabu huwa hawachaguliwi hao) nk
Lakini hatuna hata chembe ya maendeleo, nami naongezea, hao hao mafisadi na wezi ndio tunawapa kura ati, na wala hata hatuchoki.
Hivi ni kweli tumerogwa???
Kwa nini tuna amini bila ushirikina basi hatuwezi kushinda uchaguzi?
Mimi kwa kweli sijarogwa, wale wajinga ambao huuza kura zao kwa pilau tu ndio waliorogwa.
Nimetema mate pwaaaa!

Thursday, May 27, 2010

Uchokozi wa Venus Williams


Hivi karibuni Venus Williams alizusha gumzo pale alipoingia kwenye mashindano ya tennis akiwa amevaa bukta inayobana ambayo ina rangi karibu sawa na ngozi yake, kiasi kwamba waliokuwa wanamuangalia katika michapo ya tennis walikuwa wakipata hisia kama vile hajavaa kitu.
Kuna baadhi walilalamika sana!
Kama una macho mazuri kama ya kwangu utaiona bukta vyema, lakini ukiamua kutokuiona, basi utaishiwa na la kusema.

Monday, May 17, 2010

Mumhery: Ninakukubali SanaWanablog wanaonivutia kwa kuitangaza Tanzania vyema ni wengi.

Mmoja wa wanaonivutia sana ni Mumhery ambaye yupo pichani hapo juu na ambaye anaishi Japan.

Pamoja na kuwa anajishughulisha kujikimu na maisha, lakini bidhaa zake ambazo ni za ubunifu wa hali ya juu hulitangaza vyema bara la Afrika hususan Tanzania.

Makala zake za biashara na matukio, hazikosi kionjo cha nyumbani, na cha kufurahisha zaidi, huwatumia wajapani wenyewe kwa kudhihirisha ya kuwa mavazi hayo yanawapendeza pia.

Natoa changamoto kwa watanzania wengine kumuunga mkono Mumhery kwa juhudi za kukuza uchumi wetu, wa nchi na kuitangaza Tanzania.

Mumhery hongera sana!

Monday, May 10, 2010

Hongera Chelsea


Nawapa pongezi wapenzi wote wa Chelsea kwa kuweza kutwaa ubingwa kwa kubahatisha!!!

Msinishambulie kwa hilo.

Mabao 8 - 0 ni mengi lakini mkicheza na timu yenye wachezaji pungufu... mlikuwa na haki ya kuwabamiza.
Man. united kazeni buti tena, msimu ujao una kazi kweli kweli.

Gunners... msimu wenu kuvunja watu miguu sasa.. ha ha haaaa

Tuesday, May 4, 2010

With a Light Touch

A thief-catching-machine was invented in Japan and tested in various parts of the world.
The results were very interesting!

In USA, it caught 30 thieves in 30 minutes;
In UK, it caught 20 thieves in 35 minutes;
In Kenya, it caught 30,000 thieves in 20 minutes and;
In Nigeria, the machine itself was stolen in just 5 minutes!!!

Wednesday, April 21, 2010

Mji wa Mwanza Wavutia

Katiak kupitia vibaraza vya watu, nimekutana na picha nyingi za mji wa Mwanza, ambazo kwa kweli zimenivutia sana hasa ujengaji wa majumba katika milima yenye mawe na pia usafi wa mji wenyewe

Nimeona si vibaya nikitoa chache hapa kwangu ili na nyie msikose uhondo.
Kwa picha zaidi angalia hapa
Kisha tafuta kwenye post za April 2010

Sunday, April 18, 2010

Happy Sunday


I wish you the happiest sunday

Saturday, April 17, 2010

Wakimbizi wa Burundi Wazaana kama Kuku Huko Kigoma

Jamani hii ni hatari!!

Kambi hii ya Warundi yenye watu 60,000 tu, lakini kila mwezi wanazaa watoto 200!
Kwa mwendo huu kweli tutafika, au ndio hao jamaa wataendelea kutuharibia mazingira yetu huko Kigoma?

Inabidi serikali ichukue hatua za dharura na kuwaelimisha hao wakimbizi, wasidhani huku ndio mahali pa kuzalisha jeshi la kuja kwenda kupigana miaka 20 ijayo huko kwao.

Au ndio msema wa zamani ya kuwa utajiri wa maskini ni watoto. Na kazi kuu ya maskini kufyatua watoto!

Kwa kweli kasi ya kuzaana kwa wakimbizi inatisha.

Nawatakia weekend njema.

Tuesday, April 13, 2010

Tusiwe Mazumbukuku Mwaka Huu. No Pilau

Majuzi CCM imeanzisha mpango wa uchangiaji wa kuongeza kipato kwa sababu ya uchaguzi kwa kutumia SMS.
Kunapotokea majanga watu hawataki kusikia michango, lakini kwa sasa wanachangia watu wenye mabilioni wakati wachangiaji wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku!!

Chama hiki kinadai watu wote wenye mapenzi mema na chama hiki wakichangie ili kiendelee kuwa madarakani.

Lakini hakisemi kitawasaidiaje watu hao wanaokichangia mabilioni ya pesa, wakati kwa miaka yote ambapo kiko madarakani kimekuwa kikitoa ahadi nyingi sana wakati wa kampeni za uchaguzi, na kikishaingia madarakani ndio basi, barabara zitakuja kutifuliwa na kujaa vumbi uchaguzi ukikaribia.

Kwa nyie mliobahatika kuwahi kupiga kura, tena zaidi ya mara moja na kumchagua mtu yule yule ambaye huwa haonekani jimboni mpaka uchaguzi ukikaribia, huwa mna maana gani?

Mwaka huu, hii itakuwa ni fursa yangu ya kwanza kumcahgua mtu ambaye ninafikiri ndiye atakayetukomboa. SITAJALI KUWA KATOKA SIJUI CHAMA GANI AU NINI. Kwani uchaguzi wangu na watu wengine ndio unaotoa mwelekeo wa nchi yetu.

Nawasihi vijana wenzangu tujitokeze kwa wingi na kuwatupilia mbali waongo na wezi wakubwa wa haki zetu na tuchague mtu atakayetuletea maendeleo.

Huu ndio ulikuwa ukimya wangu mkuu, nilikuwa natafakari sana!!

Tuesday, March 23, 2010

Vivazi vya Brazil

Sijui ni hali ya joto sana au basi mavazi kutokupewa umuhimu nchini Brazil, kwani akina dada wanavaa mavazi ya muaibisho kupita kiasi.
Ukiangalia mavazi wanayovaa wakati wa Samba carnival festival utachoka mwenyewe.

Sasa na huu mtindo wa kupanda pikipiki uhuku wakiwa robo tatu ...., sijui wanajisikiaje, au ndio mambo ya coccaine imeshapanda vichwani???!!!


Ingekuwa mitaa ya uarabuni sijui ingekuwaje?

Mpaka sasa sijapata picha halisi ya vivazi hivi, na kama kweli vinakubalika mitaani huko wakati wote.

Nawatakiajumanne njema wasomaji wangu wote!

Friday, March 19, 2010

Mambo ya Ubunifu na Biashara

Kwa wale wanaotaka kupata starehe ya uhakika baada ya kuchoka na kazi nyingi au kero nyingi sana, basi watu wa Costa Rica wamebuni hoteli ya aina yake ikiwa katika muundo wa ndege ya boeing.
Hapa ni chumba cha mapumziko na runinga ikiwapo


Hiki ni chumba cha kulala
Kila kizuri ni gharama, kwa hapa usiku mmoja unalipa kati ya pauni za uingereza 200 - 300!
Wenye pesa zenu nendeni huko
Nawatakia wikend njema

Monday, March 15, 2010

Hebu Tutafakari Hapa


Kwa wale wanaojua mambo ya kidini...
Hivi kubatiza kwa kumdumbukiza mtu kwenye maji na kumwagia maziwa kichwani na usoni (Kwney picha hii jamaa kalenga jicho la muumini) ni dhehebu gani vile wanafanya hivi.
Kuna yeyote anayejua maana ya kufanya hivi?
Mtanisamehe maana mimi ni mpagani, na mambo ya dini hayajanikaa sana. Huwa najitahidi kusoma biblia angalau huwa naweza kuelewa kilichoandikwa kwani kinasomeka kwa elimu yangu, koran imecharangwa mwandiko nisiouelewa hata chembe!!

Monday, March 8, 2010

Changamoto ya Siku ya Wanawake Duniani 2010

Leo ni furaha kwetu kusherekea siku yetu Duniani ingawa tunakabiliwa na vikwazo vingi tu.
Mfumo wa kisiasa Duniani na hasa katika nchi zinazoendelea ndio unaochangia kwa kiasi fulani kuendelea kuwafanya wanawake wawe katika hali duni.

Kilio cha wanawake wengi katika sehemu nilizopata kuzisikia leo, ni kule Uganda ambapo wanawake wamelalamika vifo kwa akina mama wajawazito vinazidi kuongezeka

Huko Kongo wamelalamika unyanyasaji na ubakaji

Dar es salaam wameonyesha wadi ya watoto wakiwa wamerundikwa kitanda kimoja na huku wazazi (akina mama) wanalala chini

Lakini nimeipenda changamoto ya Rais Kikwete aliyesema mabadiliko ya mwanamke yatatoka kwa mwanamke mwenyewe, na hiyo ndio falsafa amabayo mimi binafsi ninayoiamini.

Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa nasoma utafiti mmoja uliofanyika huko Luanda, mji mkuu wa Angola kwenye kijarida kiitwacho HEALTH CARE FOR WOMEN INTERNATIONAL: Adaptation of health care seeking behaviour during child birth.

Habari niliyoikuta humo ilinifungua zaidi uelewa wangu. Kwani ilichambua kikamilifu kutoka kwa akina mama wenyewe sababu iliyokuwa inawafanya wasiende kujifunguia hospitali

Sababu zifuatazo ndio zilizotolewa:
 • Walikuwa wakijisikia wageni na uoga hospitali tofauti na wanapokuwa nyumbani, kwani wengine walikuwa wametoka kwenye maeneo ya vita, na walikuwa na wasiwasi wa kuvamiwa tena wakiwa hospitali
 • Gharama za hospitali zilikuwa ni kubwa na hazieleweki (labda hongo)
 • Kulikuwa hakuna watu wa kukaa nao ambao wamewazoea kama wanapokuwa nyumbani ukizingatia na kauli za wauguzi na mlolongo mzima wa kulazwa
 • Lugha chafu za wauguzi kwenye chumba cha leba, wakati mwingine wazazi watarajiwa kuzabwa makofi wakati wa uchungu
 • Kufanyiwa upasuaji bila wazazi wenyewe kuelimishwa na wakati mwingine walikuwa wanaambiwa sababu ndogo tu
 • Wale walikokuwa na historia ya kuzaa usiku tu walikuwa wanaogopa kwenda hospitali uchungu ukianza kwa kuogopa majambazi njiani.
 • Kulazimishwa kukaa mkao fulani wakati wa kujifungua wakati wao wanapendelea mwingine
 • kuongezwa njia wakati mtoto anatoka wakati wakunga wa jadi hawafanyi hivyo
 • Kwa ujumla walikuwa wanapendelea nyumbani kwa sababu kuna watu wanaowajua karibu, na kuwafariji uchungu ukizidi, na pia wanakuwa na muhudumu muda wote tofauti na chumba cha leba.

Lakini pia kuna taarifa ya sehemu fulani nchini kwetu ya kuwa wakunga wa jadi huwalazimisha mabinti wakajifungulie nyumbani, na wakati wa ujauzito kuwapa mabinti dawa za kutapika ili watoto wasiwe wakubwa ili iwe rahisi kujifungulia nyumbani katoto kadogo!
Pia uhaba wa vifaa vya kujifungulia, huchangia wakina mama kwenda hospitali dakika za majeruhi kuepuka vifaa vyao kutumiwa na watu wengine, pia kukwepa kero za lugha chafu za manesi na kubanana kitanda kimoja huku kila mtu akiguna kivyake.

Tunajua umuhimu wa mzazi mtarajiwa, kwani anatarajiwa kuleta kiumbe hai kingine duniani. Mimi nafikiri tuchukue kumbukumbu hii ya siku ya wanawake kwa kuboresha eneo hili, kwani linachukua sehemu kubwa ya vifo ambavyo vinatokea kwa watu ambao sio wagonjwa (Kuwa na ujauzito sio ugonjwa).

Wednesday, March 3, 2010

Dhana ya kuwatumia Vibaya Watoto


Watoto ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu. Watoto huleta furaha ndani ya nyumba na kwa familia pia.
Watoto wanatakiwa kutunzwa na kufunzwa adabu nzuri mapema ili waje kuwa waadilifu kikazi na kimaisha
Kelele zao huwa kero pale unapokuwa nao, lakini wakiondoka na kubaki mpweke unaweza kutamani kulia :-(
Lakini watu wamekuwa wanawatumia watoto vibaya, kama:
 • Kuwageuza chambo cha kupatia pesa hasa kwa omba omba kuwaanika juani au kuwaweka vifua wazi wakati wa baridi kwenye mitaa ili wapewe kitu kidogo na wapita njia
 • Kuwashindisha njaa ili wakonde na kuwafanya watu wawaonee huruma na kutoa chochote, lakini anayefaidi ni mlezi au muanikaji
 • Kuwageuza marching guys kwa kuwapa bidhaa ndogo ndogo na kwenda kuziuza mitaani, kama vile njugu, karanga na hata mchicha
 • Kuwageuza ngao wakati wa kutokuelewana kati ya wazazi, mwingine anaweza kumtesa mzazi mwenziwe kisaikolojia kwa kumkatalia kumwona mtoto pale wanapotengana, au mwingine kugeuza mashine ya kutengeneza pesa kwa kudai mayumizi ya mtoto wakati anazitumia mwenyewe
 • Wengine wanaanzisha vituo vya watoto yatima lakini kiasi kikubwa cha msaada uingia wanakula wao kwa kujijengea majumba makubwa ya kupangisha, na kila siku kupiga domo la kuomba misaada
 • Wengine wanawatumia kwenye vita, na kuwafundisha kuua
 • Wengine wamewageuza kama sehemu ya kujistarehesha kimapenzi. Kwa hapa natema mate kabisa pwaaaa!
Watoto laiti wangekuwa wanaweza kupata kijarida cha kujieleza... Wangesema mengi.
Labda ndio maana hao hapo kwenye picha wameanza kupoza mawazo mapema kabla shida za dunia hazijawaangukia :-(

Friday, February 26, 2010

Tabu na Mashaka


Kama wewe ulikuwa unafikiria uko kwenye shida na mahangaiko makubwa, basi jaribu kujiweka kwenye nafasi ya hawa watu waliopo katika mafuriko huku mvua ikiendeelea kunyesha!

Thursday, February 25, 2010

Tuesday, February 23, 2010

Ndoa: Nani ni Chachu ya Ndoa Kufungwa - Mwanume au Mwanamke?

Wikend kulikuwa na mabishano kati ya wanandoa waliojumuika pamoja kwa chakula cha mchana

Ubishi ulikuwa ni wa aina yake, kwani walikuwa wanabishana ni nani hasa anamvuta mwingine na kuweza kufikia maamuzi ya kuoana.
Wanaume walikuwa wao ndio huanzisha juhudi hiyo, kwa kuwatongoza wanawake, na hata wakati mwingine kuchapia na uwongo mradi wawavute wananwake na kukubaliwa, kwa hiyo walikuwa wanadai wao ndio vinara au chachu ya ndoa zote zinazofanyika

Wanawake walikiri ya kuwa wanaume wanaongoza kwa utongozaji, lakini ni kama vile mvua unaponyesha, kwanai matone yanayoanguka chini ni mengi sana kuliko yale yanayompata mtu atembeaye mvuani, pamoja na kwamba anaweza kuloa chapachapa, lakini ni asilimia ndogo sana ya matone ndio yaliyomdondokea.
Kwa hiyo mwanaume asijidai ndio chanzo cha kuwezesha kumshawishi mwanamke waoane, isipokuwa ni uamuzi wa mwanamke kumkubali mtu ili wfunge ndoa.

Wanawake waliendelea kusema ya kuwa wao ndio hasa wachaguzi wa mtu wampendaye, kwani wakioridhika na mwanaume fulani, basi hujilengesha kwa makusudi na kwa usiri mkubwa bila mwanaume kujua, huku wakisubiria tu arushe kaneno ili wasijeonekana ya kuwa wao ndio wametongoza, maana ati mwanamke kumuanza mwanaume kwa mila za kiafrika kunaleta picha mbaya!

Ubishi huu ulinivutia sana japo mie niliona kama vile bado ni maji marefu kwangu.

Natumaini wazoefu wa shughuli hii wanafahamu zaidi.

Sunday, February 14, 2010

I want You to be My Valentine


I just want to wish you the happiest Valentine's day.
Nawapenda wasomaji wangu wote, na hii ndio ishara pekee ninayoweza kuuonyesha msomaji mpenzi wangu wa blogu hii.
Mungu awabariki wote mliousoma huu ujumbe.
Happy Valentine's day!!

Friday, February 12, 2010

Ujumbe wa wikiend: Mazoezi ya Mwili


Tunaaza wikendi Jamani.
Tusisahau kufanya mazoezi, hasa kwa wale mlio zoea kuendesha magari kwenda kazini kila siku.
Afya ya viungo ni muhimu sana kujiweka fit na kuongeza muda wa kuishi.
Kufanya mazoezi sio gharama kama kutibu maradhi yanayosababishwa na kutokufanya mazoezi.
Wikend njema jamani

Monday, February 8, 2010

Mheshimiwa Rais, Hapo Umechemka!

Mimi binafsi huwa sipendi siasa achilia mbali kuongea mambo yanayohusu wanasiasa au viongozi wa serikali.
Lakini leo ni tofauti kidogo.......

Leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari kwenye runinga fulani ya kwetu Bongo.
Habari ilikuwa inahusu Mhesh Rais akitembelea sehemu zilizokumbwa na mafuriko hapo mtaa ya Wakaguru na Waluguru ili kujionea mwenyewe hali halisi ya athari za mafuriko.

Kwa hilo nimemsifia sana, kwa moyo wa kuwatembelea wanachi walioathirika na majanga kama haya ya mafuriko.

Katika hotuba yake, kuna jambo ambalo limenisononesha, pale alipokuwa akiwaagiza watendaji wasiwahamishe watu ambao wameshaanza kujenga makao yao japo ya muda, kasema wasipelekwe kwenye mahema, jambo lililonisononesha, ni pale alipokuwa akitoa hotuba yake mbele ya watu wa rika zote, akisema ya kuwa watu wasihamishwe maana kwenye mahema ni kama vile kutaleta matatizo kwa wazazi kugombana na watoto wao ati wakikaa ndani wataziba...., maana wazazi watalalamika ati mtoto hataki kwenda kucheza nje, na watakuwa wanawalazimisha watoto waende wakacheze nje......

Kwa uelewa wangu, mheshimiwa Rais alikuwa anazungumzia jambo moja tu, kwa wazazi kuwalazimisha watoto waende nje kucheza maana yake ........

Je? Mheshimiwa rais ameona watu hao kupoza machungu, basi ni ku....... tu au??!!
Au amewaona je watu hao, kwamba wanahusudu ..... sana, basi kaamua kuzungumza hadharani mbele ya hata na watoto?

Pamoja na kuwa watu walicheka, akiwemo mhesh Rais mwenyewe, ningekuwa mimi ningewaomba radhi wananchi hao.

Friday, February 5, 2010

Huku ni Kuchanganyikiwa!

Naomba nitangulize samahani kwa wale watakaokereka na picha hizi.

Inasikitisha kuona ndugu zetu wanapoenda kunengua ngwasuma basi hata ile aibu ya mwanamke wanaitupa mbali.
Nini kisa cha kupanda jukwaani ukiwa mtupu kiasi hiki!!!

Picha hizi zinasambaa kama moto wa nyikani, mimi nimezipata kutoka mtandaoni.
Naona ni bora hata angevaa nguo ya kusitiri hizo sehemu alizoziacha wazi, na zile sehemu alizofunika ndio angeziacha wazi tujue ya kuwa ankumbukia asili ya enzi hizo wakati hakuna nguo.

Wednesday, February 3, 2010

Mapumziko yameisha!!

Nilikuwa nimechukua mapumziko kidogo.

Mambo ya mwaka mpya nk. Kunesanesa mduara muhimu kabla ya kuanza majukumu ya mwaka mpya.

Nimerudi kiwanjani hivi karibuni, natumaini nimesamehewa kwa kimya cha ghafla!

Thursday, January 21, 2010

Mteleza Theluji Amwaga Radhi Nje Nje


Dada mteleza kwenye theluji wa Uingereza, Gillian Cooke, amepata kisago pale alipokuwa anajiandaa kuchupa katika mashindano ya kuteleza kwenye theluji mara baada ya nguo yake aliyovaa kufumuka kwa nyuma na kumwaga wazi wazi makalio na G-string yake nyeusi.
Bahati mbaya au nzuri hakugundua hii kasoro mpaka alipokuwa amemaliza mtelezo wake ndio kwa tahayari akagundua usumbufu huo ambao ulinaswa live na kamera za waandishi wa habari.
Hili ni fundisho kwetu tupendao kuvaa skin tight, tena za mtumba. Kuna siku zitakuaibisha

Tuesday, January 19, 2010

Haiti Aid Overwhelm the Actual Supply


Haiti imekumbwa na tatizo kubwa la tetemeko la ardhi.

Wakati naangalia TV nimepata na sikitiko kubwa kuona watu wakifa ndani ya majengo walipokwama kwa sababu tu ya vifaa duni kuwaokoa.

Pia misaada mingi imekuja lakini imeshindwa kuwafikia walengwa kwa sababu ya ubove wa miundo mbinu iliyofuatia haribiko la tetemeko.

Tatizo jingine jipya ni kuwa hakuna anayesimamia ugawaji wa misaada, kila mtu anajifanya yeye ndio kinara. Wakati USA imehodhi uwanja wa ndege na hivyo kufanya ndege za misaada kutoka sehemu nyingine kushindwa kutua, Umoja wa mataifa umekuwa unajifanya ndio unasimamia ugawaji wa chakula huku ukiwa hauna jitihada zinazo onekana kwa kugawa chakula.

Naye Rais wa Haiti anadai yeye ndio kiongozi wa shughuli zote, wakati hana meno hata ya kuamua nii kiende wapi na nini cha kufanya.

Mashirika mengine yanafanya kazi kiaina bila kuwa na mipangilio ya pamoja, lakini yanashukuru kuwa hakuna masuala ya kisiasa katika kutoa misaada wakijaribu kulinganisha na sehemu kama Darfur - Sudan na kule Myanmar walipojaribu kwenda wakati wa majanga.

Wanaoumia zaidi ni wananchi wa kwaida, inasikitisha sana kwa kweli

Soma hapa kwa maelezo

Tuesday, January 12, 2010

Admirable Michelle Obama

I always admires Lady Michelle Obama..

Huyu mama alistahili kuwa mwanamitindo, maana anajua kuchagua nguo za kuvaa, na sijui kama huwa anarudia nguo.

Ninatamani siku moja ningepata fursa ya kutembelea ward-robe yake nikajionee mitindo mbalimbali ya nguo zake.

Wednesday, January 6, 2010

Uchumiiiiiiii


Ugonjwa mwingine kuna wakati unaweza kuwa kivutio au kuleta visa na mikasa
Hapo sijui kama mtoto anahitaji kufungwa na mbeleko!!

Tuesday, January 5, 2010

Vazi rasmi la Kidini


Mtoto mdogo akiwa katika kundi la wanawake wa kiislamu.
Sijui kwa nini yeye naye hakuvishwa nguo za namna ile.. kama ya watu wazima

Friday, January 1, 2010

Heri ya mwaka mpya wa 2010

Nawatakia heri ya mwaka mpya 2010 kwa watu wote haswa wapenzi wa blogu.

Nipo kijijini napumzika, mtandao ni kazi kweli kuupata.

Ngoja tukusanye nguvu turudi tena kwenye ulingo.