Saturday, August 7, 2010

Uchaguzi wa Rais: Mipaka ya Rwanda Kufungwa?


Rwanda inatarajia kufanya uchaguzi wa Rais wake hapo tarehe 9 agosti 2010.

Kampeni zinasemekana kuwa za amani na hazina vurugu au shughuli nyingi kama ilivyo Kenya, Tanzania na Uganda.

Kuna uwezekano mkubwa Rais wa sasa Paul Kagame akashinda kwa kishindo kama kawaida yake. Uchaguzi uliopita, jimbo la kaskazini walimpa kura za ndiyo kwa asilimia mia moja, yaani watu wote waliopiga kura walimpa kura ya ndiyo. Nafikiri kwa Tz hiyo inahesabika kama ndoto... sasa sijui viongozi wetu sio wasafi au waadilifu?

Habari mpya tunayoisikia, ni kuwa kuanzia Jumatatu mipaka yote itafungwa, hakuna kuingia wala kutoka, sasa sijui ni mpaka lini?

Pia inasemekana ya kuwa wanyarwanda walishapigwa stop kuchukua passport mpya, hasa kwa wale wanaotaka kupata kwa mara ya kwanza miezi kadhaa iliyopita, ati wasubiri mpaka uchaguzi upite!

Hizi habari zinaweza kuwa propaganda au ni za ukweli.


Tunaombea uchaguzi wa amani huko Rwanda.

2 comments:

emu-three said...

Usalama wa nchi ni muhimu kama wanafanya hivyo kwa nia njema, na tunawatakia heri na demokrasia njema

Anonymous said...

go rwanda go rwanda go rwanda upoo juu ka mlima kili.mungu ibariki rwanda na watu wake pia waafrica wote kwa jumla.rwanda miaka misaba ijao ka hong kong vile