Friday, November 27, 2009

Michoro inavyoremba Uso na MwiliAhaaaaSio lazima kutumia gharama kubwa kuupamba uso na kuwakaribisha vibaka kukupora.

Very simple, hata kwa watoto wanapendeza, jaribu kufanya hivi siku ya sherehe ya mwanao ya kuzaliwa, utamwona jinsi atakavyo furahia, he he heee

Thursday, November 26, 2009

Hmm!! Men designs!I was attracted by these men's fashion which I came accross this websiteNi za ajabu , lakini nafikiri watu wakizijaribu kwenye award fulani wanaweza kuwa gumzo la sikuDesigner ni John Galliano, kwa wale mnaomfahamu.

Wednesday, November 25, 2009

Rihana: Kipindi cha mpitoRihana kama unavyomuona hapo juu, yupo katika kipindi kigumu, labda pia cha furaha kwa kuachana na rafiki yake katili kama wanavyomuita wengine Chris Brown.

Anajiandaa kuporomosha vitu vipya, ingawa amechelewa kidogo kuvitoa kama ilivyotarajiwa.

Mtakumbuka Chris alishitakiwa baada ya kumjeruhi vibaya Rihana katika mzozo, na watu walimshauri Rihana kuachana naye.

Monday, November 23, 2009

Tuwajibike jamani


Wikend imekwisha! Burudani imetosha, na umeliwazika vya kutosha.
Ni wakati wa kujenga nchi yako.
Jumatatu njema

Sunday, November 22, 2009

Vimini: Vinavutia au humpendezesha mdada!!


Kuna dhana moja ambayo watu wengi wanadau mwanamke kuvaa nguo/sketi fupi huwa anapendeza, na hasa anapokuwa ana umbo pana.
Swali ninalojiuliza, ni kweli huwa anapendeza au anakuwa kivutio kwenye macho ya wanaume?
Wazungu wengi huwa si wenye maumbile yenye hips pana, pale wanapovaa nguo fupiama dada hapo juu niliyebahatika kukutana naye huwa hawawapagaishi wanaume.
Jaribu kufikiria mdada mbantu hapo chini akivaa kimini kama hiki atapendeza au kuvutia?
Kazi kwako

Friday, November 20, 2009

Hips, Hips na mahips

Unene umekuwa unahusishwa na magonjwa ya moyo, lakini wataalamu wanasema si kila unene unaweza kuleta magonjwa hayo. Unene wa hips na matako pekee hauna madhara na wala hakuna haja ya kumsumbua mtu na kumwambia apunguze mlo. Pia inasemekana mapaja kuwa mapana ni njia kinga ya magonjwa hayo ya moyo.
Ila unene wa tumbo yaani kitambi ndio mbaya.

Inasemekana wanawake wenye hips pana pamoja na kwamba wana usalama kwa magonjwa ya moyo, lakini waume zao wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kwa sababu ya wasiwasi, hasa wake zao wanapolazimika kwenda kwenye semina au warsha na kulazimika kukaa huko kwa zaidi ya siku 2, huku nyuma wanaume viroho huwadunda sana na kusababisha matatizo ya moyo.

Sijui wewe unasemaje!?

Picha: Imebanduliwa kutoka kwa Masangu

Thursday, November 19, 2009

Nashukuru kuingia humu

Nafahamu mwanzo ni mgumu, lakini najua wadau mtaniunga mkono na kunisapoti ili niwe kama nyinyi.

Nitatembelea blogu zenu kujifunza mengi kutoka kwenu, naomba msinichoke.
Pia nawakaribisha sana, msiudhike na vituko hapa kwenye blogu, kila kitu ni kuelimishana, kinachoudhi, ni funzo kwa watu kwamba tusifanye hayo mambo.