Tuesday, August 17, 2010

Uteuzi wa Baadhi ya Wagombea Wabunge CCM ni Utata Mtupu

Uteuzi wa majina ya wagombea ubunge kwa CCM umekuja kwa hisia tofauti hasa baada ya baadhi ya wagombea walioshinda kura za maoni kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.
Mwakalebela ameenguliwa ati kwa sababu kakiuka maadili, yaani anatuhumiwa kwa rushwa, wakati Mramba na Chenge wana kesi mahakamani, lakini ati wanadai kuwa hawa ni watuhumiwa tu, na kesi haijaamuliwa, kwa hiyo wamepitisha majina yao. Sasa Mwakalebela yeye ameshahukumiwa au ni mtuhumiwa tu?

Mwenye bahati mbaya zaidi ni Hussein Bashe, ambaye alipata kura nyingi sana za maoni jimboni Nzega, lakini ghafla kageuzwa kuwa sio raia wa Tanzania kwa kudai kuwa wazazi wake wote walikuwa wasomali kabla ya kupewa uraia wakati Bashe akiwa na miaka 10.

Kwa sasa Bashe ana umri mkubwa tu, sio miaka 10 na nusu au 11, yaani amekuwa mtanzania mpaka hapo juzi tu ndo ati CCM wanadai sio raia.

Ilikuwaje walimpa nyadhifa mbalimbali huku wakijua sio raia wa Tanzania?
Je asingeshindwa kura za maoni, huo uraia wake ungehojiwa?
Nakumbuka wakati wa uchaguzi wa UVCCM, Bashe alienguliwa tena wakidai umri wake umezidi, wakati hapo awali, viongozi waliokuwepo akiwemo Nchimbi walichaguliwa wakiwa "vijeba".

Je ana bahati mbaya au ni makusudi?

Mimi nahisi CCM wanajua details za wanachama wao, wakiona wewe ni moto wa kuotea mbali, basi fimbo ya kwanza ni uraia. Nakumbuka Jenerali yalimkuta kama haya, Kinana pia.

Kwa nini kusubiri mtu anapoelekea kushinda, ndio mlete stori za kuwa sio raia, wakati ameishi zaidi ya miaka 40 Tanzania, na mmempa mpaka na pasi ya kusafiria na wala hakuna aliyesema kuwa huyu sio mbongo.

Sheria inasema mhamiaji akiishi kinyume cha sheria ya uhamiaji, anakamatwa mara moja na kufunguliwa mashitaka, mbona hapa hatuoni hilo?
Mwajiri wa mtu huyo, naye pia ushitakiwa kwa kosa la kumuajiri raia wa kigeni bila kufuata utaratibu, mbona CCM hawajashitakiwa kwa kosa hilo?

Nafikiri msajiri wa vyama vya siasa anapaswa kuisimamisha CCM ili wanachama wake wachunguzwe uraia :-(

Nafikiri inabidi kufanya uchunguzi wa kina, maana wakati wa mchakato wa kura za maoni, wengi tu walikuwa wanazushiwa ati sio raia wa Tanzania!!!!

Pata njia ya kujua orodha ya wagombea wateule wa CCM hapa

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Mi napata wakati mgumu sana kuyatafakari maamuzi ya ovyo ya CCM..
Wanasema Mwakalebela anawekwa kando, anatuhumiwa kwa rushwa. Lakini wapo wanaotuhumiwa kwa kuliingiza taifa hasara kubwa.

Kazi ipo. Hapo ndipo unapoona kuna umuhimu wa Watizedi kubadilika.

Upepo Mwanana said...

Nakubalina anawe kaka Fadhy

emu-three said...

Wenye macho wanaambiwa watizame, kwani kila jambo hutokea ili watu wajifunze! Fikiria nini kinachotokea hapo, na ni ndugu kwa ndugu, je mtu baki itakuwaje

Simon Kitururu said...

Mmmmh!