Wednesday, December 16, 2009

Monday, December 14, 2009

Michezo mingine Kwa Akina Dada!!


Mimi ni mpenzi sana wa chokleti, nikiiona mate hujaa mdomoni.

Lakini nilipoona haya mashindano ya kupigana mieleka huku mwili mzima ukiwa umepakawa chokleti, ....... nilisikia kama vile kutema.
Mavazi wanayovaa pia... ambayo ndio kama ndoano ya kumwangusha mtu, nisikilizie ikivutwa watu wanavyoachwa @*%?


Hawa ni akina dada huko Belarus wakiwa katika mieleka hiyo ya ukichaa, ati na watazamaji wapo kushuhudia, na tena sijui wanalipia!!

Picha kwa hisani ya travelNews

Wednesday, December 9, 2009

Viongozi wa Tanzania na Uhuru wa wa-Tanganyika

Mimi huwa sipendi kabisa kuzungumzia mambo ya politiki, lakini kwa sababu Tanzania inasheherekea miaka 48 ya uhuru wake...

Watanzania wengi wamekuwa na mtazamo tofauti na viongozi wao. Mfano mzuri ni kamahuyo ng'ombe dume au bull, ambaye anafananishwa na kiongozi mbele ya watu, ya kuwa yeye anataka kuwajeruhi wananchi wanomtunza kwa kumwekea kibanda asishambuliwe na simba usiku, na wakati huo huo huyo bull yeye anawaona wananchi kama kikaragosi, na kuwakimbiza kila anapowaona na kuwajeruhi, bila kufikiria ya kuwa ni hao hao watu ndio wanaomlinda kwa kumpa lishe,makazi na matibabu.

Fikiria hilo li-bull likikuumiza, linajali? au litatafuta mwingine wa kujeruhi. Ndio raslimali zetu zinavyo jeruhiwa

Ni wazo tu la siku ya uhuru.

Sunday, December 6, 2009

Vazi la skeletonMambo ya ubunifu wa mavazi mh! Sijui designers wamekosa cha kubuni!!

Hapa ni maonyesho ya mavazi ya ki-aina, nguo hii imetengeenezwa na kunakshiwa kwa picha ya mifupa (skeleton). Sifahamu mtu ataivalia wapi nguo kama hii

Kazi ipo

Thursday, December 3, 2009

Tiger Wood - Mzinzi?Inasemekana Tiger Wood alipopata ajali ya gari hivi karibuni, alikuwa ameyoka kupata kipigo kutoka kwa mkewe.
Sababu ni kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake.
Mkewe, Elin Nordegren ambaye ana miaka 29 sasa (tunashea birth day) na mwenye watoto wawili, zamani alikuwa mtu wa mitindo na urembo huko kwao Sweden, inasemekana alikasirishwa sana na kitendo hicho.Elin, Enzi hizo za u-model
Wood ambaye ni mkimya sana, inasemekana hajaweka wazi habari hii, ingawa kuna fununu kuwa ni kweli kwa namna fulani alikiuka kiapo!
Kwa ajali hiyo Tiger amesababisha hasara ya dola 3,500 kwenye gari na mti alio-ugonga!!

Haya ndio matatizo ya kuwa mtu maarufu, watu wanakufuata kama inzi ....

Tuesday, December 1, 2009

Sexy designs!Halafu mtu unasingizia ati umevaa sketi!!!
He eh he heeeeHivi nikijaribu nguo kama hizi itakuwaje, figure yangu, mhhh sijui