Tuesday, February 23, 2010

Ndoa: Nani ni Chachu ya Ndoa Kufungwa - Mwanume au Mwanamke?

Wikend kulikuwa na mabishano kati ya wanandoa waliojumuika pamoja kwa chakula cha mchana

Ubishi ulikuwa ni wa aina yake, kwani walikuwa wanabishana ni nani hasa anamvuta mwingine na kuweza kufikia maamuzi ya kuoana.
Wanaume walikuwa wao ndio huanzisha juhudi hiyo, kwa kuwatongoza wanawake, na hata wakati mwingine kuchapia na uwongo mradi wawavute wananwake na kukubaliwa, kwa hiyo walikuwa wanadai wao ndio vinara au chachu ya ndoa zote zinazofanyika

Wanawake walikiri ya kuwa wanaume wanaongoza kwa utongozaji, lakini ni kama vile mvua unaponyesha, kwanai matone yanayoanguka chini ni mengi sana kuliko yale yanayompata mtu atembeaye mvuani, pamoja na kwamba anaweza kuloa chapachapa, lakini ni asilimia ndogo sana ya matone ndio yaliyomdondokea.
Kwa hiyo mwanaume asijidai ndio chanzo cha kuwezesha kumshawishi mwanamke waoane, isipokuwa ni uamuzi wa mwanamke kumkubali mtu ili wfunge ndoa.

Wanawake waliendelea kusema ya kuwa wao ndio hasa wachaguzi wa mtu wampendaye, kwani wakioridhika na mwanaume fulani, basi hujilengesha kwa makusudi na kwa usiri mkubwa bila mwanaume kujua, huku wakisubiria tu arushe kaneno ili wasijeonekana ya kuwa wao ndio wametongoza, maana ati mwanamke kumuanza mwanaume kwa mila za kiafrika kunaleta picha mbaya!

Ubishi huu ulinivutia sana japo mie niliona kama vile bado ni maji marefu kwangu.

Natumaini wazoefu wa shughuli hii wanafahamu zaidi.