Tuesday, March 23, 2010

Vivazi vya Brazil

Sijui ni hali ya joto sana au basi mavazi kutokupewa umuhimu nchini Brazil, kwani akina dada wanavaa mavazi ya muaibisho kupita kiasi.
Ukiangalia mavazi wanayovaa wakati wa Samba carnival festival utachoka mwenyewe.

Sasa na huu mtindo wa kupanda pikipiki uhuku wakiwa robo tatu ...., sijui wanajisikiaje, au ndio mambo ya coccaine imeshapanda vichwani???!!!


Ingekuwa mitaa ya uarabuni sijui ingekuwaje?

Mpaka sasa sijapata picha halisi ya vivazi hivi, na kama kweli vinakubalika mitaani huko wakati wote.

Nawatakiajumanne njema wasomaji wangu wote!

Friday, March 19, 2010

Mambo ya Ubunifu na Biashara

Kwa wale wanaotaka kupata starehe ya uhakika baada ya kuchoka na kazi nyingi au kero nyingi sana, basi watu wa Costa Rica wamebuni hoteli ya aina yake ikiwa katika muundo wa ndege ya boeing.
Hapa ni chumba cha mapumziko na runinga ikiwapo


Hiki ni chumba cha kulala
Kila kizuri ni gharama, kwa hapa usiku mmoja unalipa kati ya pauni za uingereza 200 - 300!
Wenye pesa zenu nendeni huko
Nawatakia wikend njema

Monday, March 15, 2010

Hebu Tutafakari Hapa


Kwa wale wanaojua mambo ya kidini...
Hivi kubatiza kwa kumdumbukiza mtu kwenye maji na kumwagia maziwa kichwani na usoni (Kwney picha hii jamaa kalenga jicho la muumini) ni dhehebu gani vile wanafanya hivi.
Kuna yeyote anayejua maana ya kufanya hivi?
Mtanisamehe maana mimi ni mpagani, na mambo ya dini hayajanikaa sana. Huwa najitahidi kusoma biblia angalau huwa naweza kuelewa kilichoandikwa kwani kinasomeka kwa elimu yangu, koran imecharangwa mwandiko nisiouelewa hata chembe!!

Monday, March 8, 2010

Changamoto ya Siku ya Wanawake Duniani 2010

Leo ni furaha kwetu kusherekea siku yetu Duniani ingawa tunakabiliwa na vikwazo vingi tu.
Mfumo wa kisiasa Duniani na hasa katika nchi zinazoendelea ndio unaochangia kwa kiasi fulani kuendelea kuwafanya wanawake wawe katika hali duni.

Kilio cha wanawake wengi katika sehemu nilizopata kuzisikia leo, ni kule Uganda ambapo wanawake wamelalamika vifo kwa akina mama wajawazito vinazidi kuongezeka

Huko Kongo wamelalamika unyanyasaji na ubakaji

Dar es salaam wameonyesha wadi ya watoto wakiwa wamerundikwa kitanda kimoja na huku wazazi (akina mama) wanalala chini

Lakini nimeipenda changamoto ya Rais Kikwete aliyesema mabadiliko ya mwanamke yatatoka kwa mwanamke mwenyewe, na hiyo ndio falsafa amabayo mimi binafsi ninayoiamini.

Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa nasoma utafiti mmoja uliofanyika huko Luanda, mji mkuu wa Angola kwenye kijarida kiitwacho HEALTH CARE FOR WOMEN INTERNATIONAL: Adaptation of health care seeking behaviour during child birth.

Habari niliyoikuta humo ilinifungua zaidi uelewa wangu. Kwani ilichambua kikamilifu kutoka kwa akina mama wenyewe sababu iliyokuwa inawafanya wasiende kujifunguia hospitali

Sababu zifuatazo ndio zilizotolewa:
  • Walikuwa wakijisikia wageni na uoga hospitali tofauti na wanapokuwa nyumbani, kwani wengine walikuwa wametoka kwenye maeneo ya vita, na walikuwa na wasiwasi wa kuvamiwa tena wakiwa hospitali
  • Gharama za hospitali zilikuwa ni kubwa na hazieleweki (labda hongo)
  • Kulikuwa hakuna watu wa kukaa nao ambao wamewazoea kama wanapokuwa nyumbani ukizingatia na kauli za wauguzi na mlolongo mzima wa kulazwa
  • Lugha chafu za wauguzi kwenye chumba cha leba, wakati mwingine wazazi watarajiwa kuzabwa makofi wakati wa uchungu
  • Kufanyiwa upasuaji bila wazazi wenyewe kuelimishwa na wakati mwingine walikuwa wanaambiwa sababu ndogo tu
  • Wale walikokuwa na historia ya kuzaa usiku tu walikuwa wanaogopa kwenda hospitali uchungu ukianza kwa kuogopa majambazi njiani.
  • Kulazimishwa kukaa mkao fulani wakati wa kujifungua wakati wao wanapendelea mwingine
  • kuongezwa njia wakati mtoto anatoka wakati wakunga wa jadi hawafanyi hivyo
  • Kwa ujumla walikuwa wanapendelea nyumbani kwa sababu kuna watu wanaowajua karibu, na kuwafariji uchungu ukizidi, na pia wanakuwa na muhudumu muda wote tofauti na chumba cha leba.

Lakini pia kuna taarifa ya sehemu fulani nchini kwetu ya kuwa wakunga wa jadi huwalazimisha mabinti wakajifungulie nyumbani, na wakati wa ujauzito kuwapa mabinti dawa za kutapika ili watoto wasiwe wakubwa ili iwe rahisi kujifungulia nyumbani katoto kadogo!
Pia uhaba wa vifaa vya kujifungulia, huchangia wakina mama kwenda hospitali dakika za majeruhi kuepuka vifaa vyao kutumiwa na watu wengine, pia kukwepa kero za lugha chafu za manesi na kubanana kitanda kimoja huku kila mtu akiguna kivyake.

Tunajua umuhimu wa mzazi mtarajiwa, kwani anatarajiwa kuleta kiumbe hai kingine duniani. Mimi nafikiri tuchukue kumbukumbu hii ya siku ya wanawake kwa kuboresha eneo hili, kwani linachukua sehemu kubwa ya vifo ambavyo vinatokea kwa watu ambao sio wagonjwa (Kuwa na ujauzito sio ugonjwa).

Wednesday, March 3, 2010

Dhana ya kuwatumia Vibaya Watoto


Watoto ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu. Watoto huleta furaha ndani ya nyumba na kwa familia pia.
Watoto wanatakiwa kutunzwa na kufunzwa adabu nzuri mapema ili waje kuwa waadilifu kikazi na kimaisha
Kelele zao huwa kero pale unapokuwa nao, lakini wakiondoka na kubaki mpweke unaweza kutamani kulia :-(
Lakini watu wamekuwa wanawatumia watoto vibaya, kama:
  • Kuwageuza chambo cha kupatia pesa hasa kwa omba omba kuwaanika juani au kuwaweka vifua wazi wakati wa baridi kwenye mitaa ili wapewe kitu kidogo na wapita njia
  • Kuwashindisha njaa ili wakonde na kuwafanya watu wawaonee huruma na kutoa chochote, lakini anayefaidi ni mlezi au muanikaji
  • Kuwageuza marching guys kwa kuwapa bidhaa ndogo ndogo na kwenda kuziuza mitaani, kama vile njugu, karanga na hata mchicha
  • Kuwageuza ngao wakati wa kutokuelewana kati ya wazazi, mwingine anaweza kumtesa mzazi mwenziwe kisaikolojia kwa kumkatalia kumwona mtoto pale wanapotengana, au mwingine kugeuza mashine ya kutengeneza pesa kwa kudai mayumizi ya mtoto wakati anazitumia mwenyewe
  • Wengine wanaanzisha vituo vya watoto yatima lakini kiasi kikubwa cha msaada uingia wanakula wao kwa kujijengea majumba makubwa ya kupangisha, na kila siku kupiga domo la kuomba misaada
  • Wengine wanawatumia kwenye vita, na kuwafundisha kuua
  • Wengine wamewageuza kama sehemu ya kujistarehesha kimapenzi. Kwa hapa natema mate kabisa pwaaaa!
Watoto laiti wangekuwa wanaweza kupata kijarida cha kujieleza... Wangesema mengi.
Labda ndio maana hao hapo kwenye picha wameanza kupoza mawazo mapema kabla shida za dunia hazijawaangukia :-(