Tuesday, August 31, 2010

Maadili ya Uchaguzi Tanzania ni Yapi?

Huu ni msimu wa kisiasa Tanzania

Ni vigumu kufunga midomo kuzungumzia siasa hata kama hupendelei mambo ya siasa.


Kuna kitu ambacho sikielewi kuhusu sheria mpya ya matumizi ya fedha katika uchaguzi wa Tanzania, hasa pale wanapozungumzia matumizi ya lugha au kwa kifupi kufuata maadili.


Inaonekana kuna baadhi ya vyama wakihusishwa na tuhuma fulani za ufisadi, hata kama tuhuma hizo hizi zilisababisha watu katika chama hicho kujiuzulu na wengine kushitakiwa, kwa sasa wanakuja juu.


Kwa anaye elewa hayo maadili, naomba anielimishe!!

Tuesday, August 24, 2010

Ni Ukweli Huu

Lazima tukubali.

Tunavuna tulichopanda, na tunakula kile tunachokifikia.
Kama hufikii vilivyo nona, kuna sharti lazima ulitimize... Maana yake, ni lazima uhangaike.

Nawatakia siku njema

Tuesday, August 17, 2010

Uteuzi wa Baadhi ya Wagombea Wabunge CCM ni Utata Mtupu

Uteuzi wa majina ya wagombea ubunge kwa CCM umekuja kwa hisia tofauti hasa baada ya baadhi ya wagombea walioshinda kura za maoni kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.
Mwakalebela ameenguliwa ati kwa sababu kakiuka maadili, yaani anatuhumiwa kwa rushwa, wakati Mramba na Chenge wana kesi mahakamani, lakini ati wanadai kuwa hawa ni watuhumiwa tu, na kesi haijaamuliwa, kwa hiyo wamepitisha majina yao. Sasa Mwakalebela yeye ameshahukumiwa au ni mtuhumiwa tu?

Mwenye bahati mbaya zaidi ni Hussein Bashe, ambaye alipata kura nyingi sana za maoni jimboni Nzega, lakini ghafla kageuzwa kuwa sio raia wa Tanzania kwa kudai kuwa wazazi wake wote walikuwa wasomali kabla ya kupewa uraia wakati Bashe akiwa na miaka 10.

Kwa sasa Bashe ana umri mkubwa tu, sio miaka 10 na nusu au 11, yaani amekuwa mtanzania mpaka hapo juzi tu ndo ati CCM wanadai sio raia.

Ilikuwaje walimpa nyadhifa mbalimbali huku wakijua sio raia wa Tanzania?
Je asingeshindwa kura za maoni, huo uraia wake ungehojiwa?
Nakumbuka wakati wa uchaguzi wa UVCCM, Bashe alienguliwa tena wakidai umri wake umezidi, wakati hapo awali, viongozi waliokuwepo akiwemo Nchimbi walichaguliwa wakiwa "vijeba".

Je ana bahati mbaya au ni makusudi?

Mimi nahisi CCM wanajua details za wanachama wao, wakiona wewe ni moto wa kuotea mbali, basi fimbo ya kwanza ni uraia. Nakumbuka Jenerali yalimkuta kama haya, Kinana pia.

Kwa nini kusubiri mtu anapoelekea kushinda, ndio mlete stori za kuwa sio raia, wakati ameishi zaidi ya miaka 40 Tanzania, na mmempa mpaka na pasi ya kusafiria na wala hakuna aliyesema kuwa huyu sio mbongo.

Sheria inasema mhamiaji akiishi kinyume cha sheria ya uhamiaji, anakamatwa mara moja na kufunguliwa mashitaka, mbona hapa hatuoni hilo?
Mwajiri wa mtu huyo, naye pia ushitakiwa kwa kosa la kumuajiri raia wa kigeni bila kufuata utaratibu, mbona CCM hawajashitakiwa kwa kosa hilo?

Nafikiri msajiri wa vyama vya siasa anapaswa kuisimamisha CCM ili wanachama wake wachunguzwe uraia :-(

Nafikiri inabidi kufanya uchunguzi wa kina, maana wakati wa mchakato wa kura za maoni, wengi tu walikuwa wanazushiwa ati sio raia wa Tanzania!!!!

Pata njia ya kujua orodha ya wagombea wateule wa CCM hapa

Saturday, August 7, 2010

Uchaguzi wa Rais: Mipaka ya Rwanda Kufungwa?


Rwanda inatarajia kufanya uchaguzi wa Rais wake hapo tarehe 9 agosti 2010.

Kampeni zinasemekana kuwa za amani na hazina vurugu au shughuli nyingi kama ilivyo Kenya, Tanzania na Uganda.

Kuna uwezekano mkubwa Rais wa sasa Paul Kagame akashinda kwa kishindo kama kawaida yake. Uchaguzi uliopita, jimbo la kaskazini walimpa kura za ndiyo kwa asilimia mia moja, yaani watu wote waliopiga kura walimpa kura ya ndiyo. Nafikiri kwa Tz hiyo inahesabika kama ndoto... sasa sijui viongozi wetu sio wasafi au waadilifu?

Habari mpya tunayoisikia, ni kuwa kuanzia Jumatatu mipaka yote itafungwa, hakuna kuingia wala kutoka, sasa sijui ni mpaka lini?

Pia inasemekana ya kuwa wanyarwanda walishapigwa stop kuchukua passport mpya, hasa kwa wale wanaotaka kupata kwa mara ya kwanza miezi kadhaa iliyopita, ati wasubiri mpaka uchaguzi upite!

Hizi habari zinaweza kuwa propaganda au ni za ukweli.


Tunaombea uchaguzi wa amani huko Rwanda.

Monday, August 2, 2010

Kura Za Maoni CCM: Vurugu Tupu

Jamani hizi kura za maoni za CCM mbona zimejaa rafu sana...

Kweli chama hiki ni safi au kimejaa uchafu, yaani madai ya hongo, vurugu, na kila aina ya mambo yasiyo kimaadili katika kuomba ridhaa ya kuwakilisha chama ili kupata viongozi yanasikika.

Cha ajabu na watuhumiwa wa ufisadi, kuna wanaojizolea kura nyingi tu. Tutafika kweli?!!!

Nini mwelekeo wa siasa zetu.


Mimi naogopa kabisa. Itabidi niitumie kura yangu vizuri kumchagua kiongozi wa kweli. Wananchi tusiangushane