Friday, February 26, 2010

Tabu na Mashaka


Kama wewe ulikuwa unafikiria uko kwenye shida na mahangaiko makubwa, basi jaribu kujiweka kwenye nafasi ya hawa watu waliopo katika mafuriko huku mvua ikiendeelea kunyesha!

Thursday, February 25, 2010

Tuesday, February 23, 2010

Ndoa: Nani ni Chachu ya Ndoa Kufungwa - Mwanume au Mwanamke?

Wikend kulikuwa na mabishano kati ya wanandoa waliojumuika pamoja kwa chakula cha mchana

Ubishi ulikuwa ni wa aina yake, kwani walikuwa wanabishana ni nani hasa anamvuta mwingine na kuweza kufikia maamuzi ya kuoana.
Wanaume walikuwa wao ndio huanzisha juhudi hiyo, kwa kuwatongoza wanawake, na hata wakati mwingine kuchapia na uwongo mradi wawavute wananwake na kukubaliwa, kwa hiyo walikuwa wanadai wao ndio vinara au chachu ya ndoa zote zinazofanyika

Wanawake walikiri ya kuwa wanaume wanaongoza kwa utongozaji, lakini ni kama vile mvua unaponyesha, kwanai matone yanayoanguka chini ni mengi sana kuliko yale yanayompata mtu atembeaye mvuani, pamoja na kwamba anaweza kuloa chapachapa, lakini ni asilimia ndogo sana ya matone ndio yaliyomdondokea.
Kwa hiyo mwanaume asijidai ndio chanzo cha kuwezesha kumshawishi mwanamke waoane, isipokuwa ni uamuzi wa mwanamke kumkubali mtu ili wfunge ndoa.

Wanawake waliendelea kusema ya kuwa wao ndio hasa wachaguzi wa mtu wampendaye, kwani wakioridhika na mwanaume fulani, basi hujilengesha kwa makusudi na kwa usiri mkubwa bila mwanaume kujua, huku wakisubiria tu arushe kaneno ili wasijeonekana ya kuwa wao ndio wametongoza, maana ati mwanamke kumuanza mwanaume kwa mila za kiafrika kunaleta picha mbaya!

Ubishi huu ulinivutia sana japo mie niliona kama vile bado ni maji marefu kwangu.

Natumaini wazoefu wa shughuli hii wanafahamu zaidi.

Sunday, February 14, 2010

I want You to be My Valentine


I just want to wish you the happiest Valentine's day.
Nawapenda wasomaji wangu wote, na hii ndio ishara pekee ninayoweza kuuonyesha msomaji mpenzi wangu wa blogu hii.
Mungu awabariki wote mliousoma huu ujumbe.
Happy Valentine's day!!

Friday, February 12, 2010

Ujumbe wa wikiend: Mazoezi ya Mwili


Tunaaza wikendi Jamani.
Tusisahau kufanya mazoezi, hasa kwa wale mlio zoea kuendesha magari kwenda kazini kila siku.
Afya ya viungo ni muhimu sana kujiweka fit na kuongeza muda wa kuishi.
Kufanya mazoezi sio gharama kama kutibu maradhi yanayosababishwa na kutokufanya mazoezi.
Wikend njema jamani

Monday, February 8, 2010

Mheshimiwa Rais, Hapo Umechemka!

Mimi binafsi huwa sipendi siasa achilia mbali kuongea mambo yanayohusu wanasiasa au viongozi wa serikali.
Lakini leo ni tofauti kidogo.......

Leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari kwenye runinga fulani ya kwetu Bongo.
Habari ilikuwa inahusu Mhesh Rais akitembelea sehemu zilizokumbwa na mafuriko hapo mtaa ya Wakaguru na Waluguru ili kujionea mwenyewe hali halisi ya athari za mafuriko.

Kwa hilo nimemsifia sana, kwa moyo wa kuwatembelea wanachi walioathirika na majanga kama haya ya mafuriko.

Katika hotuba yake, kuna jambo ambalo limenisononesha, pale alipokuwa akiwaagiza watendaji wasiwahamishe watu ambao wameshaanza kujenga makao yao japo ya muda, kasema wasipelekwe kwenye mahema, jambo lililonisononesha, ni pale alipokuwa akitoa hotuba yake mbele ya watu wa rika zote, akisema ya kuwa watu wasihamishwe maana kwenye mahema ni kama vile kutaleta matatizo kwa wazazi kugombana na watoto wao ati wakikaa ndani wataziba...., maana wazazi watalalamika ati mtoto hataki kwenda kucheza nje, na watakuwa wanawalazimisha watoto waende wakacheze nje......

Kwa uelewa wangu, mheshimiwa Rais alikuwa anazungumzia jambo moja tu, kwa wazazi kuwalazimisha watoto waende nje kucheza maana yake ........

Je? Mheshimiwa rais ameona watu hao kupoza machungu, basi ni ku....... tu au??!!
Au amewaona je watu hao, kwamba wanahusudu ..... sana, basi kaamua kuzungumza hadharani mbele ya hata na watoto?

Pamoja na kuwa watu walicheka, akiwemo mhesh Rais mwenyewe, ningekuwa mimi ningewaomba radhi wananchi hao.

Friday, February 5, 2010

Huku ni Kuchanganyikiwa!

Naomba nitangulize samahani kwa wale watakaokereka na picha hizi.

Inasikitisha kuona ndugu zetu wanapoenda kunengua ngwasuma basi hata ile aibu ya mwanamke wanaitupa mbali.
Nini kisa cha kupanda jukwaani ukiwa mtupu kiasi hiki!!!

Picha hizi zinasambaa kama moto wa nyikani, mimi nimezipata kutoka mtandaoni.
Naona ni bora hata angevaa nguo ya kusitiri hizo sehemu alizoziacha wazi, na zile sehemu alizofunika ndio angeziacha wazi tujue ya kuwa ankumbukia asili ya enzi hizo wakati hakuna nguo.

Wednesday, February 3, 2010

Mapumziko yameisha!!

Nilikuwa nimechukua mapumziko kidogo.

Mambo ya mwaka mpya nk. Kunesanesa mduara muhimu kabla ya kuanza majukumu ya mwaka mpya.

Nimerudi kiwanjani hivi karibuni, natumaini nimesamehewa kwa kimya cha ghafla!