Nina maswali mengi sana ninajiuliza kwa nchi yetu ya Tanzania....Yanakuja haswa pale uchaguzi wa Rais na wabunge unapokaribia.
Watu wanapotangaza azma ya kugombea mathalani ubunge, utashangaa aliye na jimbo anaanza kugaagaa na vyombo vya habari, mara apeleke vitisho na kumtaka yule anayetaka kugombea ati ajitoe, au asichukue form ya uchaguzi
Lakini si uongo, nasikia wakati huu waganga wa jadi wana soko zuri sana, na ndio wakati wao wa kivuno toka kwa politicians wajinga.
Naogopa kutamka jina la wananchi ambao huwapa wanasiasa wajinga kura, labda wewe msomaji unaweza kuwa na jina zuri.
Jana nilimsikia Pinda akisema hivi watanzania tumerogwa????? Kwa sababu fursa zote tunazo za kujiendeleza, mali ghafi, madini, mito, maziwa, vivutio, amani, viongozi safi na wazuri ( cha ajabu huwa hawachaguliwi hao) nk
Lakini hatuna hata chembe ya maendeleo, nami naongezea, hao hao mafisadi na wezi ndio tunawapa kura ati, na wala hata hatuchoki.
Hivi ni kweli tumerogwa???
Kwa nini tuna amini bila ushirikina basi hatuwezi kushinda uchaguzi?
Mimi kwa kweli sijarogwa, wale wajinga ambao huuza kura zao kwa pilau tu ndio waliorogwa.
Nimetema mate pwaaaa!
