Haiti imekumbwa na tatizo kubwa la tetemeko la ardhi.
Wakati naangalia TV nimepata na sikitiko kubwa kuona watu wakifa ndani ya majengo walipokwama kwa sababu tu ya vifaa duni kuwaokoa.
Pia misaada mingi imekuja lakini imeshindwa kuwafikia walengwa kwa sababu ya ubove wa miundo mbinu iliyofuatia haribiko la tetemeko.
Tatizo jingine jipya ni kuwa hakuna anayesimamia ugawaji wa misaada, kila mtu anajifanya yeye ndio kinara. Wakati USA imehodhi uwanja wa ndege na hivyo kufanya ndege za misaada kutoka sehemu nyingine kushindwa kutua, Umoja wa mataifa umekuwa unajifanya ndio unasimamia ugawaji wa chakula huku ukiwa hauna jitihada zinazo onekana kwa kugawa chakula.
Naye Rais wa Haiti anadai yeye ndio kiongozi wa shughuli zote, wakati hana meno hata ya kuamua nii kiende wapi na nini cha kufanya.
Mashirika mengine yanafanya kazi kiaina bila kuwa na mipangilio ya pamoja, lakini yanashukuru kuwa hakuna masuala ya kisiasa katika kutoa misaada wakijaribu kulinganisha na sehemu kama Darfur - Sudan na kule Myanmar walipojaribu kwenda wakati wa majanga.
Wanaoumia zaidi ni wananchi wa kwaida, inasikitisha sana kwa kweli