Friday, November 20, 2009

Hips, Hips na mahips

Unene umekuwa unahusishwa na magonjwa ya moyo, lakini wataalamu wanasema si kila unene unaweza kuleta magonjwa hayo. Unene wa hips na matako pekee hauna madhara na wala hakuna haja ya kumsumbua mtu na kumwambia apunguze mlo. Pia inasemekana mapaja kuwa mapana ni njia kinga ya magonjwa hayo ya moyo.
Ila unene wa tumbo yaani kitambi ndio mbaya.

Inasemekana wanawake wenye hips pana pamoja na kwamba wana usalama kwa magonjwa ya moyo, lakini waume zao wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kwa sababu ya wasiwasi, hasa wake zao wanapolazimika kwenda kwenye semina au warsha na kulazimika kukaa huko kwa zaidi ya siku 2, huku nyuma wanaume viroho huwadunda sana na kusababisha matatizo ya moyo.

Sijui wewe unasemaje!?

Picha: Imebanduliwa kutoka kwa Masangu

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmhhh! mimi sisemi kitu kwa sasa nasubiri kwanza!