Mimi binafsi huwa sipendi siasa achilia mbali kuongea mambo yanayohusu wanasiasa au viongozi wa serikali.
Lakini leo ni tofauti kidogo.......
Leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari kwenye runinga fulani ya kwetu Bongo.
Habari ilikuwa inahusu Mhesh Rais akitembelea sehemu zilizokumbwa na mafuriko hapo mtaa ya Wakaguru na Waluguru ili kujionea mwenyewe hali halisi ya athari za mafuriko.
Kwa hilo nimemsifia sana, kwa moyo wa kuwatembelea wanachi walioathirika na majanga kama haya ya mafuriko.
Katika hotuba yake, kuna jambo ambalo limenisononesha, pale alipokuwa akiwaagiza watendaji wasiwahamishe watu ambao wameshaanza kujenga makao yao japo ya muda, kasema wasipelekwe kwenye mahema, jambo lililonisononesha, ni pale alipokuwa akitoa hotuba yake mbele ya watu wa rika zote, akisema ya kuwa watu wasihamishwe maana kwenye mahema ni kama vile kutaleta matatizo kwa wazazi kugombana na watoto wao ati wakikaa ndani wataziba...., maana wazazi watalalamika ati mtoto hataki kwenda kucheza nje, na watakuwa wanawalazimisha watoto waende wakacheze nje......
Kwa uelewa wangu, mheshimiwa Rais alikuwa anazungumzia jambo moja tu, kwa wazazi kuwalazimisha watoto waende nje kucheza maana yake ........
Je? Mheshimiwa rais ameona watu hao kupoza machungu, basi ni ku....... tu au??!!
Au amewaona je watu hao, kwamba wanahusudu ..... sana, basi kaamua kuzungumza hadharani mbele ya hata na watoto?
Pamoja na kuwa watu walicheka, akiwemo mhesh Rais mwenyewe, ningekuwa mimi ningewaomba radhi wananchi hao.
Monday, February 8, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment