Wednesday, December 28, 2011

Tatizo la Mafuta Tanzania

Bado ninajiuliza hili tatizo la upatikanaji wa mafuta Tanzania, ni tatizo la kweli au ni janja tu ya wanaojishughulisha na biashara ya mafuta kunufaika zaidi? 
  
Kwa nini matatizo yawe yanatokea katika vipindi ambapo watu ndio wanahitaji mafuta kwa wingi, na kwa nini linakuja pale bei ya EWURA inaposhuka tu. 
 
Bado najiuliza, mbona siku za nyuma tatizo hili lilikuwa halitokei? 
 
Kila la heri katika maandalizi ya mwaka mpya wa 2012!!!!

2 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Nimekukasirikia sana wewe "Upepo" kwani mimi ni mshabiki mkubwa sana wa blogu yako. Lakini unachukua karne kabisa kutoa kauli yoyote ile.

Kwa ninini?

Mimi napenda blogu yako na nataka kusoma chochote kile unachokiwaza.

Nipe pumba nitasoma tu tena nitakujibu!

Lakini haya mambo ya kukaa kwako kimya nami kwa upande wangu nikiwa nasubiri mwezi mzima kusoma ya kwako, siku moja utakuta kwa blogu ziliezagaa nimempata mpenzi mwingine shauri yako!

Kuhusu mafuta hadimu; sidhani serikali itaruhusu utapeli. Sijui Watanzania wanasemaje, kwani mimi naongea kama "mgeni", mwenyeji wa Afrika Kusini!

Upepo Mwanana said...

Tehe tehe.
Karibu sana kusoma habari za hapa na pale. Tatizo ni muda wa kukaa na kuandika ndio unanitupa mkono. Japo ninajitahidi.
Labda mwaka huu ninaweza kufanikiwa kwa kiasi fulani.