Friday, December 2, 2011

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Tsvangirai Aachana na mke Mpya Baada ya Siku 12 tu

Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, ameachana na mkewe ambaye ni mfanyabiashara tajiri nchini Zimbabwe Bi Lorcadia Karimatsenga Tembo mwenye miaka 39. 
 
Anadai chanzo ni kuingiliwa na vyombo vya usalama na kujaribu kumchafua kisiasa! Pia, anamshuku mkewe kuwa alikuwa anashirikiana na wana usalama ili kupanga njama za kumharibia kisiasa, kwani... at mkewe alikwenda kwa wazazi wake(Mke) bila kumtaarifu Waziri Mkuu (Mume). Hivyo kutokana na hayo, uhusiano wote umevurugika na hauwezi kusuluhishwa tena. 
  
Inadaiwa alikuwa amekwishalipa dola za kimarekani 36,000 na ng'ombe 10 kama mahali, lakini kwa kuvunja ndoa hii imebidi alipe dola 10,000 kama fidia kwani mke wake huyo alikuwa tayari ni mjamzito na alikuwa na watoto mapacha.

Pata habari kwa kimombo kwenye link hii

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kaaazi kwelikweli siku kumi na mbili tu? ha ha haaa...

Goodman Manyanya Phiri said...

Hii yaonyesha waziwazi ni aina gani ya mwehu watu tunaowaita "Wazee wa kisiasa wenye heshima zao". Sasa wewe Samson unakwenda kumtongoza Delila unashangaa shangaa nini anapowaita kaka zake wakunyoe? Mimi sikupi kura yangu ningekuwa Mzimbabwe!

chib said...

Watu hawa wana pesa nyingi za kutapanya eh!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Wanasiasa hawa hawana jipya.

Krismasi njema na mwaka wenye heri kwako na familia yako pamoja na wapendwa wako.

Upepo Mwanana said...

Ahsante MMN. Na kwako pia