Wednesday, December 9, 2009

Viongozi wa Tanzania na Uhuru wa wa-Tanganyika

Mimi huwa sipendi kabisa kuzungumzia mambo ya politiki, lakini kwa sababu Tanzania inasheherekea miaka 48 ya uhuru wake...

Watanzania wengi wamekuwa na mtazamo tofauti na viongozi wao. Mfano mzuri ni kamahuyo ng'ombe dume au bull, ambaye anafananishwa na kiongozi mbele ya watu, ya kuwa yeye anataka kuwajeruhi wananchi wanomtunza kwa kumwekea kibanda asishambuliwe na simba usiku, na wakati huo huo huyo bull yeye anawaona wananchi kama kikaragosi, na kuwakimbiza kila anapowaona na kuwajeruhi, bila kufikiria ya kuwa ni hao hao watu ndio wanaomlinda kwa kumpa lishe,makazi na matibabu.

Fikiria hilo li-bull likikuumiza, linajali? au litatafuta mwingine wa kujeruhi. Ndio raslimali zetu zinavyo jeruhiwa

Ni wazo tu la siku ya uhuru.

6 comments:

Faith S Hilary said...

Yaani tuko same page lol! Mie naona miaka inaenda tu lakini nothing happened kwamba we should be proud of...and I love the concept of the bull!

chib said...

Habari imenigusa, lakini na Candy!! bull concept, ha ha haa

John Mwaipopo said...

dada wakikusikia wanasiasa-viongozi sijui utawabebea mbeleko gani. Very good kwa kweli.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nadhani mfano wa "bull" umetumiwa vibaya na sidhani kama ni taswira inayoweza hasa kuakisi tabia za viongozi wetu. Mchezo huo wa kukimbiza hawa ma"bull" (ambao ni wa kimila kule Uhispania) unapigiwa makelele sana na watetea haki za wanyama. Hilo "bull" limekuzwa na kunenepeshwa kwa lengo la kustarehesha watu kwa kuwafukuza. Wakati mwingine, ili kulifanya licharuke, pembe zake humwagiwa mafuta ya taa na kisha kutiwa kiberiti. Ma"bull" haya hucharuka vibaya sana na wakati mwingine hata kuua watazamaji - lakini ni kwa sababu ya woga au maumivu. Na sidhani kama hii ndiyo taswira halisi inayoakisi viongozi wetu kama Mwalimu Nyerere na wengineo.

Hata kama taswira hii ya Bull ingekuwa na ukweli wo wote, ni kweli kwamba viongozi wetu wote wana tabia hiyo ya u"bull". Sisi watazamaji tumefanya nini kuhakikisha kwamba hawa ma"bull" hawatuvamii, kutushambulia na hata kutupotezea maisha?

Tazama ukatili wanaofanyiwa hawa ma"bull" katika clip hii (kuanzia dakika ya 3:22) uone.

http://www.youtube.com/watch?v=kH0S3pev2qg

Upepo Mwanana said...

It is horrible!!!!

Anonymous said...

nice post. thanks.