Thursday, December 3, 2009

Tiger Wood - Mzinzi?Inasemekana Tiger Wood alipopata ajali ya gari hivi karibuni, alikuwa ameyoka kupata kipigo kutoka kwa mkewe.
Sababu ni kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake.
Mkewe, Elin Nordegren ambaye ana miaka 29 sasa (tunashea birth day) na mwenye watoto wawili, zamani alikuwa mtu wa mitindo na urembo huko kwao Sweden, inasemekana alikasirishwa sana na kitendo hicho.Elin, Enzi hizo za u-model
Wood ambaye ni mkimya sana, inasemekana hajaweka wazi habari hii, ingawa kuna fununu kuwa ni kweli kwa namna fulani alikiuka kiapo!
Kwa ajali hiyo Tiger amesababisha hasara ya dola 3,500 kwenye gari na mti alio-ugonga!!

Haya ndio matatizo ya kuwa mtu maarufu, watu wanakufuata kama inzi ....

5 comments:

Chib said...

Ni kweli, taabu ya umaarufu ndio ipo hapo

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ameshalikoroga huyu baba na moto umemwakia kweli hapa Marekani. Nimeligusia hili suala hapa - ingawa lengo langu hasa ni kumakinikia utafiti wa wanasayansi ambao unaonyesha kwamba uzinzi umefumwa katika maumbile ya wanyama karibu wote - akiwemo binadamu. Kwa hivyo tusishangae mambo kama haya yanapotokea. Tazama hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/12/are-men-wired-to-cheat-sasa-ni-zamu-ya.html

Upepo Mwanana said...

Hiyo makala nimeipitia, naogopa kutoa komenti, maana naweza kushambuliwa... lol..
Nakushukuru Masangu kwa makala hiyo

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Unaogopa kutoa komenti? Eti kwa kuwa utashambuliwa? Na nani? Enzi hizi? Pole!

Mzee wa Changamoto said...

Mie bado natafakari anachomueleza mkewe wakiwa ndani. Maana najua atalipwa ili amsindikize kwenye sherehe za kijamii lakini kunyumba kukoje?
Mnatenga vitanda?
Mnalala mzungu wa nne?
Kazi ipo hapa