Monday, March 21, 2011

Tanzania: Chama Tawala ni kipi?

Naomba kusaidiwa kwenye utata huu.
Nifahamuvyo mimi, ni kuwa chama tawala ni kile kinachoshikilia dola, kwa maana ya kwamba ndicho kinachotoa kiongozi mkuu mwenye mamlaka ya serikali. Kwa maana nyingine ndio kiongozi wa kiserikali wa nchi hiyo. Ambaye anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba.
Hata kwenye nchi zinazo ongozwa kifalme (na kimalkia pia).
Vyama vya upinzani vina wajibu mmoja mkuu, nao ni kukisoa chama tawala pale kinapo endesha mambo ndivyo sivyo....

Kwa Tanzania mimi inanikanganya pale ninapojua ya kuwa chama hiki
ndicho chenye hatamu na ndicho chama tawala. Kimekuwa mstari wa mbele katika kujikita uongozini kwa juhudi zote kama vile kusukuma greda kwa kutumia fito.

Lakini kuna chama hiki

Kimekuwa kikishutumiwa sana na chama kileee juu ya kuwa kinataka kuleta uvunjifu wa amani kwa kuwaeleza watanzania waliolala usingizi mkubwa ya kuwa wananyonywa na kupelekwa pabaya. Na kuwa serikali yao haina jipya la kuwaletea kimaendeleo baada ya miaka 50 ya kuwa madarakani, hivyo waamke na kuchagua chama kitakacholeta maendeleo. Mimi nahisi huo ndio ukweli na maana ya upinzani. Kukosoa chama tawala pale kinapokosea.

Sasa huyu ndugu

naye anakuja juu na kumkashifu mpinzani wa serikali. Huyu ndugu anadai tena ati Chama chenye mamlaka ya wananchi kinataka kupinduliwa na chama kingine kwa kuwaamsha waliolala usingizi, ati wakiamka kwa ghafla watakuwa na hasira na mtawala wao kwa kugutuka kuwa walipokuwa wamelala, walikuwa wanapigwa bakora sana kama vile hawana akili nzuri..
Huyu ndugu kaungana na mwingine ambaye ana bendera ya bluu ambayo haipatikani mitandaoni na kumshambulia huyo anayekuja kwa nguvu za uma. Naye anadai mwenye dola anataka kupinduliwa kwa staili ya kuwaamsha watu wajue ya kuwa wanatembea bila nguo barabarani.
Sasa hapo ninachanganyikiwa, kwani sijui chama tawala ni nyundo au ni antenna.
Kama wewe unajua kisayansi, basi nielezee!!
Angalizo: Mimi sio mwanasiasa, ila ni mpenda maendeleo na ukweli


2 comments:

emu-three said...

Siasa , siasa ...nakumbuka sana lile swali tuliloulizwa o-level, lilisema hivi `siasa ni uongo wenye ukweli ndani yake....jadili'
Nia na madhumuni ya vyama vyote ni kuchukua dola, na kile kilichopo madarakani ni kulinda ili kiendelee kuwepo madarakani. Kwahiyo pamoja na kuwajibka kama chama tawala, pia kina majukumu ya kuhakikisha kuwa vyama vingine havina nguvu, kwa kila mbinu.
Vyama vya upinzani nia na lengo lake ni kuwa ipo siku vitaingia madarakani, na haviwezi vikaingia vyote, ni kimojawapo, kwahiyo wakati vinakimbizana kuitafuta ikulu, lazima kuna kuchezeana rafu, ili `kitangulie, komojawapo'
Kwahiyo yote yanayotokea ndio hiyo mbinu,ya kupigana ngwala, kusukumana, ...
Cha muhimu kwa sisi wanachama, wapenzi , wananchi, nk ni kuangalia nyendo za hivi vyama, ili mwisho wa siku ukifika wa uchaguzi tunakuwa na maamuzi sahihi, ...kawasababu atakayetawala akivurunda watakaoumia ni sisi...tuwe makini kwa hili!

Anonymous said...

Kweli kabisa emu-three