Thursday, March 10, 2011

Umakini wa Watanzania!


Waziri wa nishati na madini, Mhesh Ngeleja, wa tatu kutoka kushoto akisikiliza kwa makini hoja katika mkutano mmojawapo wa kimataifa.

Kulia kwake yupo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mh. Kikwete.

Picha kutoka kwa Mnyonge Mnyongeni....

5 comments:

emu-three said...

Shukurani kutuletea hii habari, nashukuru sana kwa kunitembeela mara kwa mara `upepo mwanana'

John Mwaipopo said...

mmoja alipigwa picha kama hiyo kule bungeni dodoma. akajitetea kuwa hakulala bali alikuwa akiombea amani nchi ya tanzania. inawezekana pia huyo pichani hakulala bali naye alikuwa katika 'aina' mpya ya maombezi kwa taifa la tanzania ili masuala anuai hasa yale yaliyo chini yake ya umeme yaishe. mungu ibariki tanzania na viongozi wake

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mimi nadhani kamera imemkuta akiwa ameangalia chini tu. Nashindwa kuamini kwamba kweli anaweza kuamua kuutandika usingizi mbele ya bosi wake tena mchana kweupe namna hii dunia ikimwangalia.

Kijana huyu anaongoza wizara yenye changamoto kuliko zote. Hata akiutandika usingizi mimi sitamlaumu!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa Taarifa hii!!

Anonymous said...

Hata kama alikuwa macho, lakini picha hii imeichangamsha siku yangu