Thursday, March 24, 2011

Kuwa Mwangalifu Katika Ujana wako

Fiona Walker bado anajutia picha hii aliyopigwa mwaka 1976 akiwa bado ni kijana wakati huo akiwa na miaka 18 tu.  
Alikubali kupiga picha hiyo kumfurahisha mpenzi wake wa kiume ambaye alikuwa na tamaa ya kuwa mpiga picha maarufu.
Ilibidi aazime nguo na reki ya mchezo wa tenisi ili aonekane kama kweli alikuwa mchezaji mahili.     
    
Rafiki yake wa kiume aliweza kupata pauni kama laki mbili na nusu kwa kuruhusu kuuzwa kwa picha hiyo ambayo ilitolewa nakala kama milioni 2 baada ya kuonekana ilikuwa maarufu sana.  
  
Sasa hivi Fiona akiiona picha hii, anajuta na kusema kama angejua, katu asingekubali kupiga picha hiyo.  
  
Soma habari hii hapa

3 comments:

emu-three said...

Vitu vya kuuweka mwili wako namna hiyo hutakiwi ukubali, kama mpo mnapendana kwanini msiangaliane ndani...picha za nini? Utazalilika bure

Anonymous said...

Ni kweli emu-three. Sasa imekuwa majuto ni mjukuu. Ha ha haaa

Malkiory Matiya said...

Waswahili walisema majuto ni mjukuu.