Thursday, December 23, 2010

Maisha ni jinsi mtu unavyojipanga.
Kipendezacho machoni pako, ni kwa jinsi unavyokiona wewe mwenyewe, kwani mwingine kinaweza kuwa kinamuudhi, japo wewe wakipenda sana.

Kila kitu kwa mfano wake waweza kukifanya kikafanana na akili yako inavyotaka, na ndio maana hao ndege watatu warukao angani katika picha hii, unaweza kufananisha na kitu fulani unachokifahamu, au unachotaka kiwe.

Kwa ufupi nataka kuwaasa kuwa maisha ni chaguo lako mwenyewe, furaha itakuwepo, iwapo utakubali hali uliyonayo na kujaribu kuitunza kama ilivyo au kuiboresha mwenyewe.

Tunapoelekea kuanza mwaka mpya wa 2011, basi tuzingatie hayo.

Merry Christmas and Happy New Year 2011!
Photo from Oman Collective Intelligence

5 comments:

SIMON KITURURU said...

Bonge la ujumbe!

Merry Christmas and Happy New Year 2011 kwako pia mtu wangu!

Yasinta Ngonyani said...

Upepo mwanana! Ahsante kwa ujumbe mzuri. Unajua mie nilipoangalia niliona kama naona taswira ya simba na baadae kama ya mtu na mwisho......Noeli njema na pia Mwaka 2011 uwe wa amani kwako:-)

emu-three said...

Kweli maisha ni wewe mwenyewe, kupanga au kuchagua, kuyajenga au kuyabomoa! sikukuu njema

chib said...

Happy new year Upepo

Upepo Mwanana said...

Ahsanteni sana!!