Thursday, January 20, 2011

Jamani, Nipo

Wapendwa wangu!!!

Mwaka huu, sijui kwa sababu ulianza na 1.1.11 nami ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa, basi sijui nilichanganyikiwa!!!

Magimbi na matembele naona yalikuwa yamenilevya, hata hivyo yote ni heri, mimi ni mzima na buheri wa afya.

Nina matumaini nanyi pia mu wazima kabisa.
Nawashukuru kwa uvumilivu wenu, na cha muhimu kupita mara kwa mara kusalimia nyumba iliyokuwa haina mwenyewe.

Mungu awabariki sana!!
Tupo pamoja

11 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kwanza kheri sana ya mwaka mpaya na karibu tena . Na pila HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KUMBE MWIZI HUU TULIZAWLIWA WENGI. Ni furaha upo nasi.

Upepo Mwanana said...

Hongera Da Yasinta japo sina hakika tarehe yako ya kuzaliwa ni lini.

Fadhy Mtanga said...

swali likanichanganya sana....
yu wapi Upepo Mwanana.....
kitambo wala hajaonekana....

alaaa....!

sasa umerejea....
kisha ukatuambia....
nini unakifikiria.....

karibu tena jamvini....!

EDNA said...

Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa na heri ya Mwaka mpya 2011,

Yasinta Ngonyani said...

Ukiingia hapo Maisha na Mafanikio utakuta tarehe:-) nshatimiza mwenzio

Goodman Manyanya Phiri said...

Salaam Upepo!

Posti yako hii imenipeleka moja kwa moja rohoni mwako.

Inaelekea wewe hapo ni mtu anayejuwa namna ya kuhesabu baraka zake; na ulivyotaja tarehe yako ya kuzaliwa umenikumbusha binti yangu (DAUGHTER) aliyezaliwa tarehe 10 mwezi wa 10 mwaka 2010 dakika kasoro 10 ya saa 4 asubuhi wakati wa Afrika Kusini na sijui kama atafanana na Upepo mbona nitafurahi baba-mtu!!

Jinsi tunavyohesabu baraka badala ya magumu yetu, ndivyo tunavyozidi kubarikiwa. Nakutakia mwaka 2011 wa mafanikio zaidi pamoja na wasomaji wako (blogi yako nimegundua leo kwa kuongozwa... bila yeye kukusudia... na "Mama Yetu Mdogo" ...nimekwishampa sifa na najua atakuja kuniponda pitia EMAIL yangu... Dada Yasinta Ngonyani).

Mbarikiwe nyote!P.S. Sijui Yasinta amekwishakujibu kuhusu tarehe yake ya kuzaliwa lakini mie najuwa tayari: NI MWEZI WA JANUARY TAREHE TANO/// Mimi mwenyewe ni mwezi waTANO tarehe NNE, mie kijana mdogo wa juzijuzi tu jamaani lakini msininyanyase: 1961! Asanteni

Yasinta Ngonyani said...

ha hahaaaaa! nimecheka mpaka mbavu zanaiuma ntakuwa na majina mangapi jamani? na halafu nilishampa jibu Upepo kuwa aende Maisha na Mafanikio na apekue na atapata jibu ni tarehe gani, ila basi sasa kaka Manyanya kakarahisishia.

emu-three said...

hongerani sana...na usijali sana, haya niyo maisha!

Upepo Mwanana said...

Jamani nawashukuruni nyote, nimekuwa na matatizo ya kupata network kama umeme wa tanesco/dowans ulivyo.
Nitapitia mabaraza yenu yote kuwasalimia mwenyezi Mungu akijalia inshaaaalah!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

karibu tena... mie nikadhani udaiwa ndo sababu ukaadimika....lol!

Upepo Mwanana said...

@Chacha, mie sio chama fulani kaka