HAYA. Mambo yanaelekea yamekwisha, leo JK ameapishwa baada ya kuchaguliwa na 27% ya watanzania waliojiandikisha kupiga kura, na 61% ya wale waliojitokeza kupiga kura!
Hapo hakuna cha kujivunia, ila kushukuru Mungu tu kuwa labda wale ambao hawakujitokeza wangepigia upinzani!
Nawapa pole wanafunzi wote wa vyuo, kwani hawakuweza kupiga kura baada ya serikali kuamua vyuo visifunguliwa hadi uchaguzi uishe ilhali wanafunzi wengi walijiandikisha wakati wakiwa chuoni. Nina hakika wengi walikuwa wanataka mabadiliko.
Ndio mwanzo huu, tunasubiri sasa mambo ya kukata rufaa na muda wa kuanza serikali mpya, tukiwa na matumaini kutakuwa na mabadiliko makubwa kiutendaji, na baadhi ya watu kupoteza ubunge wao kupitia mahakama.
Picha kutoka michuzi
Saturday, November 6, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Tusubiri hiyo serikali yake mpya kama itakuwa na mabadiliko au ndiyo yatakuwa yaleyale.
Kama alivyonena Edna, cha kusubiri ni hiyo nguvu kazi ya utendaji wa ahadi zilizosikika kwenye kampeni!
Hope haitakuwa ya kulindana nk. Maana dalili za moto ni Moshi, nahisi tumeanza kuona moshi mahali fulani. Ngoja tusubiri
Post a Comment