Friday, November 19, 2010

Kampeni za Uchaguzi 2015 Kumbe Zimesha Anza

Wakati watu wengine wanahangaika na kuona CHADEMA kitafanya nini kwenye bunge lijalo, kumbe kuna baadhi ya waheshimiwa wamekwisha anza kujipanga kwa ajili ya kugombea urais 2015.

Habari hizi ambazo bado zipo kwenye mvumo wa kichini chini zinadai kuna wanasiasa maarufu na wenye majina makubwa ambao wameshawahi kuwa mawaziri wameanza mkakati mkubwa wa kuhakikisha wanachaguliwa kuwa viongozi wa nchi.

Kati yao wapo waliowahi kuwa mawaziri na wakalazimika kujiuzuru nyadhifa zao kufuatia kashfa zilizowaandama ndani na nje ya bunge.

Yasemekana pia kuna aliyewahi kuwa waziri mkuu, na anaonekana amepania vilivyo, kwani alianza kampeni mapema hata kabla ya uchaguzi wa 2010 kufanyika. Na amekuwa hataki kujionyesha ya kuwa anawania kiti hicho, lakini ameshaunda kamati yake ya ushindi! Na anaendelea "kununua" watu ili wamuunge mkono wakati ukiwadia.
Habari hii inaweza kuwa uzushi, lakini mara nyingi kwa siasa zetu hizi chafu na safi, chochote kinawezekana.

Kwa mtazamo wetu, tunahisi wale wenye kashfa ambazo hazijafutika au kuamuliwa kihaki, wana nafasi ndogo ya kupenya ili wawanie uongozi hasa wa nchi kwa siku zijazo.

Tukumbuke kuchagua mbivu na si mbichi au pumba

3 comments:

SIMON KITURURU said...

Hongera sana kwa hao watu kwa kujua tofauti ya kuwa na ndoto na jinsi ya kutimiza ndoto.

Kumbuka kama unataka ndoto itimie kuwa na mipango ya utekelezaji mapema na sio tu kuota na kufikiri kibahatibahati itatekelezeka.

La kujifunza kutoka kwa hawa ni kuwa , kama unania yakutimiza jambofulani anza mapema kupanga, kujipanga na weka mikakati mapema ili ndoto yako itimie.:-(

Si ruksa kujifunza kitu kutokana na lolote?

Anonymous said...

Tatizo huku kwetu, mafisadi ndio huanza mikakati mapema ya kupora, na wale watu safi wanapigwa vita!

Upepo Mwanana said...

Ndipo hapooooooo