Wednesday, June 2, 2010

Watanzania Tumerogwa???

Nina maswali mengi sana ninajiuliza kwa nchi yetu ya Tanzania....
Yanakuja haswa pale uchaguzi wa Rais na wabunge unapokaribia.


Kuna kuwa na visa vingi vya watu kushikana uchawi, mara huyu kamroga huyu.
Watu wanapotangaza azma ya kugombea mathalani ubunge, utashangaa aliye na jimbo anaanza kugaagaa na vyombo vya habari, mara apeleke vitisho na kumtaka yule anayetaka kugombea ati ajitoe, au asichukue form ya uchaguzi

Kana kwamba hiyo haitoshi, utaskia vifo vya ajabu na watu wakishikana uchawi.
Lakini si uongo, nasikia wakati huu waganga wa jadi wana soko zuri sana, na ndio wakati wao wa kivuno toka kwa politicians wajinga.
Naogopa kutamka jina la wananchi ambao huwapa wanasiasa wajinga kura, labda wewe msomaji unaweza kuwa na jina zuri.
Jana nilimsikia Pinda akisema hivi watanzania tumerogwa????? Kwa sababu fursa zote tunazo za kujiendeleza, mali ghafi, madini, mito, maziwa, vivutio, amani, viongozi safi na wazuri ( cha ajabu huwa hawachaguliwi hao) nk
Lakini hatuna hata chembe ya maendeleo, nami naongezea, hao hao mafisadi na wezi ndio tunawapa kura ati, na wala hata hatuchoki.
Hivi ni kweli tumerogwa???
Kwa nini tuna amini bila ushirikina basi hatuwezi kushinda uchaguzi?
Mimi kwa kweli sijarogwa, wale wajinga ambao huuza kura zao kwa pilau tu ndio waliorogwa.
Nimetema mate pwaaaa!

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wew unasema kurogwa ikiwa na maana kuwa unaamini kurogana. ila sasa suala jingine la pinda kusema tumerogwa, basi aachie ngazi ambao hawajarogwa washike kasi

unasema wanasiasa wajinga? ujinga ninini? hivi kweli wewe sio mjinga?

katika ujinga ndiko unakotoka kutokuwa mjinga. ujinga ni muhimu

chib said...

Imani za kisiasa Bongo, kwa watu wengi wanaamini mambo ya uzandiki na fitna. Ni ukweli ambao watu hawataki kuukubali.
Nyerere alisema mficha ficha maradhi, kilio kitamfichua.
Sioni ubaya wa kutoa mawazo yako na mtazamo wako. Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na mtazamo wako

EVARIST said...

Simply,tumerogwa na aliyeturoga keshafariki...maana wanasema alokuroga akifariki ndio basi tena.Haiyumkiniki kuendelea kuwavumilia wahuni wachache wanaoipeleka nchi kusikoeleweka ilhali kuna kila sababu,nia na njia ya kuwaondoa.
Wanasiasa sio wajinga kihivyo kwa vile wanafahamu udhaifu wetu uko wapi na wanautumia ipasavyo 'kutupelekesha'.
Uhuru wa 1961 unazidi kupoteza maana yake hasa kwa vile angalau mkoloni alikuwa na excuse kuwa yeye si mtanzania kama sie (i.e. hakuwa na uchungu na nchi yetu) lakini sijui hawa wezi/mafisadi wa sasa tuwaelezeeje!
Safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu sana.Naafikiana nawe kuwa TUMEROGWA na naongezea kuwa aliyeturoga ashafariki