Monday, May 17, 2010

Mumhery: Ninakukubali Sana



Wanablog wanaonivutia kwa kuitangaza Tanzania vyema ni wengi.

Mmoja wa wanaonivutia sana ni Mumhery ambaye yupo pichani hapo juu na ambaye anaishi Japan.

Pamoja na kuwa anajishughulisha kujikimu na maisha, lakini bidhaa zake ambazo ni za ubunifu wa hali ya juu hulitangaza vyema bara la Afrika hususan Tanzania.

Makala zake za biashara na matukio, hazikosi kionjo cha nyumbani, na cha kufurahisha zaidi, huwatumia wajapani wenyewe kwa kudhihirisha ya kuwa mavazi hayo yanawapendeza pia.

Natoa changamoto kwa watanzania wengine kumuunga mkono Mumhery kwa juhudi za kukuza uchumi wetu, wa nchi na kuitangaza Tanzania.

Mumhery hongera sana!

9 comments:

mumyhery said...

Shukran Mkuu tupo pamoja

Fadhy Mtanga said...

Nami naungana nawe kumpa pongezi mama mkwe wangu.
Kila la kheri.

Yasinta Ngonyani said...

Nami sipo nyumba dada M. pongezi kwako na zidi kusonga mbele. upendo daiama

Mija Shija Sayi said...

Mumhery yuko juu, maana mara hutushtukiza kwa miavuli ya kanga, mara viatu vya kanga mara viti vya magari ya kanga.... na mengine meeengi. Kuna anayebisha kwamba si wa shoka huyu?

God bless you Mumhery.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Hongera sana. Songa mbele!

chib said...

Mumhery ongeza juhudi maradufu, watu wanaiona kazi yako. Wanaotaka wakutumie ngawira na gharama ya kutuma uwarushie product zako.

Upepo Mwanana said...

Shukrani wote kwa kuniunga mkono

Simon Kitururu said...

Hongera sana Mumyhery

Mbele said...

Hapo hakuna ubishi. Mumyhery anawakilisha utamaduni wetu kwa kiwango cha juu kabisa na pia anatuelimisha wengi tusioijua Japani. Namtakia kila la heri.