Thursday, March 3, 2011

Uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa waishtua Rwanda

Rais Sarkozy amefanya uteuzi mpya wa waziri wa mambo ya nje na kumteua Allain Juppe.

Juppe alikuwa na wadhifa huo huo wakati wa mauaji ya kimbari yaliyoikumba Rwanda mwaka 1994 na inasemekana alikuwa anaiunga mkono kwa nguvu serikali iliyokuwa madarakani Rwanda wakati wa mauaji ya watutsi.
Alidumu katika wadhifa huo hadi mwaka 1995.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Bibi Mushikiwabo, ameonyesha wasiwasi na kutofurahishwa na uteuzi huo ukuzingatia ya kuwa Rwanda na Ufaransa zimefufua mahusiano chini ya miaka 2 iliyopita, baada ya serikali ya Rais Kagame kuisusia Ufaransa kwa kile kilichokuwa kinaelezwa ya kuwa Ufaransa ilihusika moja kwa moja na uchochezi wa mauaji ya Kimbari ya watutsi, na hii ilipelekea Rwanda kubadili hata na lugha rasmi ya matumizi na kujiunga na jumuiya ya madola na kuanza kuzungumza na kufundisha shuleni kiingereza badala ya kifaransa.

Kumekuwa na wasiwasi ya kuwa watu watatoneshwa vidonda vya mauaji ya 1994 kwa uwepo wa waziri huyu kwenye wizara ile ile ambayo iliacha watu takribani milioni moja wakiuwawa kwa visasi.

3 comments:

Simon Kitururu said...

Angalau inaonyesha Waziri wa mabo ya nje anatishia kitu kwa maana Tanzania mimi hata sioni kazi ya waziri wa mambo ya nje ni nini kwakuwa Rais KIKWETE namuona kama hakuachia uwaziri wa mambo ya nje aliokuwa nao kabla hajawa Rais.

Au niambieni hivi hamstukii kama labda kuna mambo mengine yasababishayo safari za Rais wetu yalikuwa yafanywe na Waziri wa mambo ya nje?

Ila ndio hivyo tena mpaka Waziri Pinda na Magufuli naona hata mambo mengine hawaambizani maofisini na wanabishania magazetini hata katika maswala ya Bomoa bomoa!.


Mungu Ibariki AFRIKA!
Mungu Ibariki Tanzania!

chib said...

Simon umesema kweli kabisa.
Mambo mengine ni aibu kabisa, hapo ndio utagundua hatuna baraza la mawaziri linalofanya kazi pamoja.
Mkuu wetu bado ni waziri wa mambo ya nje, labda bado hajajiamini ya kuwa ndiye Mkuu zaidi :-(

malkiory said...

Hizi nchi zilizoendelea zitaendelea kutuburaza hadi lini? migogoro mingi katika Afrika chimbo lake ni wakoloni hawa, hasa kutok Ufaransa na Ubelgiji. Jaribu kufuatilia kwa umakini utakuta nchi zote zilizokuwa chini ya hawa wakoloni zina matatizo zaidi kulinganisha na zile zilizokuwa chini ya Waingereza.

Kwanza wanatuchagulia viongozi ambao vibaraka wao na baadaye wakishashiba wanaanza kuwaita madikteta. Mfano mzuri hapa ni jinsi CIA ilivyoshiriki kumuua Lumumba na kumweka pandikizi lao Mobutu. Leo hii Mobutu yumo kwenye orotha ya madikteta na viongozi waliohujumu uchumi wa nchi zao duni.