Tuesday, January 25, 2011

CCM si Shwari Hata Chembe?


Kuna fununu kuwa hali ya kifedha ndani ya chama cha mapinduzi aka CCM iko tete hasa baada ya kukumbwa na rungu la kupoteza nafasi nyingi za ubunge, na hivyo kupungua kwa kiasi kikubwa cha ruzuku ya kila mwezi.
Pia inasemekana inasakamwa na madeni katika uchaguzi uliopita na kufanya viongozi waanze kuhaha kuokoa jahazi. Inasemekana shinikizo la kujilipa kupitia Dowans ndio nia hasa ya kupata pesa kwa ajili ya kuendesha shughuli za chama, kulipa madeni na pia kukatia rufaa baadhi ya matokeo ya uchaguzi uliopita katika sehemu ambapo CCM iliangukia pua!
Pia inaaminika ya kuwa wabunge wengi wa CCM wakati wa uchaguzi walijigharimia wenyewe kwa ahadi kuwa watarejeshewa baada ya uchaguzi, kwani ruzuku za majimboni, zilielekezwa kwenye nguvu ya kugombea urais!! Lakini kutokana na kuanguka kusikotegemewa kwa CCM, hali imekuwa ni mbaya.
Pia kuna mnong'ono kuwa kuna baadhi ya makatibu na wenyeviti wa kata, na hata wilaya, malipo yameanza kuwa magumu, na kuna watu wanasingiziwa kukihujumu chama wakati wa uchaguzi ili wapate kisingizio cha kuwacheleweshea mishahara yao au hata kuwarusha!
Inasemekeana kuna wimbi la mgogoro litafumuka ndani ya kijani/njano hivi karibuni iwapo hali hii tete itaendelea, ndio maana wanahaha kulipa haraka Dowans.
Haya ni maono tu, usiulize ushahidi!!
Picha ya bendera mbinuko kutoka kwa Matukio Daima

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

haishangazi kwa kweli!!

Anonymous said...

Na bado!

emu-three said...

Wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha, ...walitakiwa kujisafisha kwa kuwaondoa `wahujumu'...wanawajua lakini wanaona aibu kwaondoa, kwani swali linakua `ni nani aliyemsafi, amnyoshee mwenzake kidole..!

Goodman Manyanya Phiri said...

Nimeandika maoni yangu hapo jana kuhusu jambo hili maana yake mimi simgeni katika ka mambo ya siasa.

Nilisema vyama vya upinzani viandike yao mazuri na mabaya kusudi tuvitambue; haisadii kamwe hao wapigakura kusoma tu udhaifu wa chama-tawala. Je kiliwahi kuishi ardhini humu kiumbe kiliekamilika?


Sjui kama maoni yangu yalikuwa makali mno ndiyo maana siyaoni mtandaoni. Au mimi mwenyewe nilishidwa kubonyeza "PUBLISH".


Ningependa sana jibu kwa mwenye blogi ilikuwakuwaje nipoteze muda bure wa kwandika kumbe "ilikuwa jasho la mbwa tu" (kama wanavyosema kwamsemo waKizulu "IZITHUKUTHUKU ZENJA")?

Je tunarudia katika ile hali ya zamani ya kale ulipokuwa lazima umrambe EDITOR wagazeti kabla ya maoni yako kutolewa?

Upepo Mwanana said...

Goodman, nahisi hukubonyeza publish, au kama ulibonyeza basi hukuakiki kama yametoka.
Maoni kwangu hakuna kizuizi, ukipublish, wewe mwenyewe ndio unakuwa wa kwanza kuyaona kabla ya mtu mwingine yeyote.
Karibu sana hata kama una mtazamo tofauti na mada, huo ndio umuhimu wa maoni na kuelimishana

Goodman Manyanya Phiri said...

Asante, Wangu!

Je, unajua kama nakupenda?!

chib said...

Kilichonivutia.. nu bendera kuwekwa upside down!