Monday, September 27, 2010

Ahadi Za Kampeni za Kisiasa TZ Zimepakwa Rangi tu

Kwa nyie mnaosikiliza kampeni za uchaguzi....

Hivi mmekwisha tafakari wenzetu wanayoahidi?

Kila mtu anaimba wimbo wake, sina hakika kama kila mtu atatimiza hayo kwenye miaka mitano anayo omba tumpe kura zetu ati atuwakilishe.

Mimi nitajenga uwanja wa ndege wa kimataifa katika kila wilaya!!!!

Mimi nitatoa elimu ya bure tangu mtoto akiwa tumboni kwa mama yake mpaka atakapo ng'oka jino la mwisho la uzeeni!!!

Mimi nitajenga meli mpya kila mto hapa Bongo, ili watu wasiliwe na mamba tena!!!!

Mimi nitahakikisha kwa muda wa wiki 2 tu, jimbo langu lote litakuwa na maji ya uhakika kwa mwaka mzima na barabara zinazopitika kila siku. (Hapo nina maana ya waenda kwa miguu, na maji ya uhakika mvua zitakapokuwa zinanyesha)

Mimi nitatoa ajira kwa watu wote, ukipata ujauzito, njoo umwandikishie mtoto wako kazi kabisa, ili akizaliwa anaanza ajira rasmi moja kwa moja...

Mimi nitatokomeza ufisadi na kilimo cha bangi kila mahali hata ikulu kama inalimwa huko!!!!!

Huo ndio mwelekeo wa kampeni, kama unatafakari, utang'amua yote, kwa jinsi ambavyo umeona mifano yangu, basi jua mwananchi wa kawaida ndio anaelezwa ahadi za namna hii.

1 comment:

chib said...

Ulikuwa unafikiria nini! Ha ha haaaa.
Umenifungua macho kiasi fulani