Wednesday, September 15, 2010

Uchaguzi Tanzania:Maswali maswaliii

Kwa haraka haraka

Nimekuwa nikfuatilia kampeni za siasa, kwani sitaki kufanya makosa wakati utakapowadia wa kumchagua kiongozi wangu wa baadaye, ukizingatia ya kuwa hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika zoezi zima la kupiga kura za kuchagua viongozi wa nci yetu,

Nimekuwa nikisikiliza kwa makini sera za wagombea mbalimbali na kuzipima kama zina ukweli, ushawishi, na pia kuangalia kama kweli zinatekelezeka au ni changa la macho.

Nahisi naanza kukata tamaa, kwani wanasiasa au wagombea nafasi za kisiasa badala ya kuhubiri sera za vyama vyao, wamekuwa mstari wa mbele kusikiliza mwenzie alisema nini, na wao kusema ya kwao kutokana na wengine walichosema hapo awali, na mwisho hakuna kampeni tena bali ni kupeana vidonge na kujibu mapigo!!!!!

Sie tunaotaka kupima sera tumejikuta tukipima nani ni bingwa wa kujibu mashambulizi, na mara ,,, hatimaye zoezi la kupiga kura litafika.. sasa hapo tutampigia kura nani?, nahisi hatutakuwa tumempata kiongozi atakayekidhi tulichotaka kusikia kabla ya kuamua.

Mpaka sasa mimi naona wengi ni wahuni na matapeli tu. Wanabembeleza wachaguliwe kwa matakwa yao binafsi. Na kwa maono yangu, naona vyama vimeelekeza nguvu na pesa nyingi kwa wagombea urais, kwani kutumia helikopta nyingi na magari utitiri kwa mgombea mmoja, wakati wagombea ubunge na udiwani wakiswaga lami ni kuonyesha ishara ya uchoyo na unafiki tu

HATUDANGANYIKIIIIIII

3 comments:

Chib said...

Nimeipakua ikiwa bado moto moto. Utaikuta na kwangu pia

Upepo Mwanana said...

Na kweli umewahi duh

emu-three said...

Umeshawahi kuhudhuria sherehe ambazo mnapakuliwa sinia moja watu wengi mnakula hapo kwa pamoja.
Nini mnachokifanya mkiwa mumeizunguka ile sinia, ni kuwa kila mmoja anakula kwake kwa juhudi, ili ashibe kabla ya wengine.
Huu ni mfano wa hizi kampeni za kutafuta kura, hawa watu wanatafuta kula, na sinia lipo moja, ni nani atasema wewe kula mpaka huku kwangu mimi nimeshashiba kabla hajashiba, na kushiba ni huko kuchukua madararaka, mwenye mkono mwepesi, mwenye kinywa kipana, na anayemeza haraka ndiye atayakula sehemu kubwa...