Matokeo ya uchaguzi mdono wa jimbo la Uzini, Zanzibar yameanza kutoa picha tofauti za kisiasa visiwani Zanzibar, mara baada ya mgombea wa CCM kuibuka kidedea kwa kuzoa zaidi ya asilimia 90 ya kura zote zilizopigwa.
Kulikuwa kunatarajiwa kuwa na mchuano mkali kati ya CCM na CUF, lakini imekuwa kinyume kwani ushindi wa CCM kupitia kwa mgombea wake Mohamed Raza ambao ulikuwa ni wa mteremko, alifuatiwa na Ally Mbarouk Mshimba wa CHADEMA na mgombea wa CUF kushika nafasi ya tatu.
Sina hakika nini kinachoendelea huko Zanzibar, lakini kwa matokeo hayo, yanaashiria kuwa CHADEMA huenda kikawa chama kitakachokuwa kinaongoza kwa upinzani huko Zanzibar.
Kwa upande wa Bara, nina wasiwasi kama CUF itaendelea kuwa na wafuasi wengi, kwani hata leo kuna wanachama zaidi ya 1,000 wamerejesha kadi zao za CUF kwa kutoridhishwa na mwenendo wa chama chao.
Wakati ni ukuta, nafikia tamati kwa leo!
Monday, February 13, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Hee, siku nyingi, sikuonagi, karibu tena
CHADEMA mbele kwa mbele
Ahsante Emu3, najikongoja kongoja
Post a Comment