Friday, April 15, 2011

Maana ya Kujivua Gamba ni Nini?

Bado sijaelewa Dhana ya kujivua gamba.

Natazama... kama vile kupaka rangi nyumba bila kubadili chochote ndani, au kama vile nyoka anavyojivua gamba lake na kuondoka akiwa na kila kitu chake ikiwa ni pamoja na sumu, tabia, ukubwa, viungo na uwezo wake wa kizazi bila kubadili hata na jinsia.

Sasa wenzetu wamejivua gamba kivipi?

Mh! Nawatakia kila la heri na mafanikio, yote iwe kwa mema ya Tanzania na watu wake!

1 comment:

Malkiory Matiya said...

Hakuna kipya zaidi ya katibu mkuu. Sure zingine ni zile zile na zimerudishwa kwa kulipa fadhila na zaidi kuendeleza utawala wa kifalme. Mnauye na January ni watoto wa makada wa CCM. Meghji na Kinana wamefanya mengi kumwingiza JK madarakani, mmoja alichota pesa za EPA na mwengine alikuwa ni meneja wa kampeni zake.