Wednesday, April 21, 2010

Mji wa Mwanza Wavutia

Katiak kupitia vibaraza vya watu, nimekutana na picha nyingi za mji wa Mwanza, ambazo kwa kweli zimenivutia sana hasa ujengaji wa majumba katika milima yenye mawe na pia usafi wa mji wenyewe

Nimeona si vibaya nikitoa chache hapa kwangu ili na nyie msikose uhondo.
Kwa picha zaidi angalia hapa
Kisha tafuta kwenye post za April 2010

Sunday, April 18, 2010

Happy Sunday


I wish you the happiest sunday

Saturday, April 17, 2010

Wakimbizi wa Burundi Wazaana kama Kuku Huko Kigoma

Jamani hii ni hatari!!

Kambi hii ya Warundi yenye watu 60,000 tu, lakini kila mwezi wanazaa watoto 200!
Kwa mwendo huu kweli tutafika, au ndio hao jamaa wataendelea kutuharibia mazingira yetu huko Kigoma?

Inabidi serikali ichukue hatua za dharura na kuwaelimisha hao wakimbizi, wasidhani huku ndio mahali pa kuzalisha jeshi la kuja kwenda kupigana miaka 20 ijayo huko kwao.

Au ndio msema wa zamani ya kuwa utajiri wa maskini ni watoto. Na kazi kuu ya maskini kufyatua watoto!

Kwa kweli kasi ya kuzaana kwa wakimbizi inatisha.

Nawatakia weekend njema.

Tuesday, April 13, 2010

Tusiwe Mazumbukuku Mwaka Huu. No Pilau

Majuzi CCM imeanzisha mpango wa uchangiaji wa kuongeza kipato kwa sababu ya uchaguzi kwa kutumia SMS.
Kunapotokea majanga watu hawataki kusikia michango, lakini kwa sasa wanachangia watu wenye mabilioni wakati wachangiaji wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku!!

Chama hiki kinadai watu wote wenye mapenzi mema na chama hiki wakichangie ili kiendelee kuwa madarakani.

Lakini hakisemi kitawasaidiaje watu hao wanaokichangia mabilioni ya pesa, wakati kwa miaka yote ambapo kiko madarakani kimekuwa kikitoa ahadi nyingi sana wakati wa kampeni za uchaguzi, na kikishaingia madarakani ndio basi, barabara zitakuja kutifuliwa na kujaa vumbi uchaguzi ukikaribia.

Kwa nyie mliobahatika kuwahi kupiga kura, tena zaidi ya mara moja na kumchagua mtu yule yule ambaye huwa haonekani jimboni mpaka uchaguzi ukikaribia, huwa mna maana gani?

Mwaka huu, hii itakuwa ni fursa yangu ya kwanza kumcahgua mtu ambaye ninafikiri ndiye atakayetukomboa. SITAJALI KUWA KATOKA SIJUI CHAMA GANI AU NINI. Kwani uchaguzi wangu na watu wengine ndio unaotoa mwelekeo wa nchi yetu.

Nawasihi vijana wenzangu tujitokeze kwa wingi na kuwatupilia mbali waongo na wezi wakubwa wa haki zetu na tuchague mtu atakayetuletea maendeleo.

Huu ndio ulikuwa ukimya wangu mkuu, nilikuwa natafakari sana!!