Tuesday, April 13, 2010

Tusiwe Mazumbukuku Mwaka Huu. No Pilau

Majuzi CCM imeanzisha mpango wa uchangiaji wa kuongeza kipato kwa sababu ya uchaguzi kwa kutumia SMS.
Kunapotokea majanga watu hawataki kusikia michango, lakini kwa sasa wanachangia watu wenye mabilioni wakati wachangiaji wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku!!

Chama hiki kinadai watu wote wenye mapenzi mema na chama hiki wakichangie ili kiendelee kuwa madarakani.

Lakini hakisemi kitawasaidiaje watu hao wanaokichangia mabilioni ya pesa, wakati kwa miaka yote ambapo kiko madarakani kimekuwa kikitoa ahadi nyingi sana wakati wa kampeni za uchaguzi, na kikishaingia madarakani ndio basi, barabara zitakuja kutifuliwa na kujaa vumbi uchaguzi ukikaribia.

Kwa nyie mliobahatika kuwahi kupiga kura, tena zaidi ya mara moja na kumchagua mtu yule yule ambaye huwa haonekani jimboni mpaka uchaguzi ukikaribia, huwa mna maana gani?

Mwaka huu, hii itakuwa ni fursa yangu ya kwanza kumcahgua mtu ambaye ninafikiri ndiye atakayetukomboa. SITAJALI KUWA KATOKA SIJUI CHAMA GANI AU NINI. Kwani uchaguzi wangu na watu wengine ndio unaotoa mwelekeo wa nchi yetu.

Nawasihi vijana wenzangu tujitokeze kwa wingi na kuwatupilia mbali waongo na wezi wakubwa wa haki zetu na tuchague mtu atakayetuletea maendeleo.

Huu ndio ulikuwa ukimya wangu mkuu, nilikuwa natafakari sana!!

No comments: