Saturday, April 17, 2010

Wakimbizi wa Burundi Wazaana kama Kuku Huko Kigoma

Jamani hii ni hatari!!

Kambi hii ya Warundi yenye watu 60,000 tu, lakini kila mwezi wanazaa watoto 200!
Kwa mwendo huu kweli tutafika, au ndio hao jamaa wataendelea kutuharibia mazingira yetu huko Kigoma?

Inabidi serikali ichukue hatua za dharura na kuwaelimisha hao wakimbizi, wasidhani huku ndio mahali pa kuzalisha jeshi la kuja kwenda kupigana miaka 20 ijayo huko kwao.

Au ndio msema wa zamani ya kuwa utajiri wa maskini ni watoto. Na kazi kuu ya maskini kufyatua watoto!

Kwa kweli kasi ya kuzaana kwa wakimbizi inatisha.

Nawatakia weekend njema.

2 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Labda raha pekee waliyonayo husababisha mazaano.
Kugeuza tendo la ndoa kama sehemu ya kutolea msongo wa mawazo (stress) ama sehemu ya kumalizia siku yako ni hatari.
Kama ni kwa mke ama mtu mmoja ndio athari za watoto kila yai linapoanza kuzaliswha na kama ni kwa wengi basi MARADHI yanakuwa zao kuu.
Tatizo kwa wakimbizi ni kuwa wana vyote. Wanazaana kwa kasi na kuambukizana kwa kasi pia. Na ni hatari kwani kuna uwezekano kuwa ni wachache kati ya wazaliwao watakaoishi kwani waathirika kwenye kambi hizo huwa wengi
Ujinga mwingine ni wa serikali yetu ambayo haiangalii mbali zaidi ya uchaguzi wa Oktoba. Wangewadhibiti hao wakimbizi kuzaliana.
Wawaangalie waMarekani wanavyohaha na jamii ya waMexico ambao wanavuka mipaka wakiwa wajawazito kisha wanajifungulia Marekani na kisheria hao watoto ni raia wa hapa Marekani. Sheria pia inatetea watoto kutotenganishwa na wazazi wao na hivyo hata kama wako hapa illegally, wana kitu kinachowapa backup na ndio maana nchi hii sasa inalia na illegal immigrants ambao wamejazana kwa mamilioni na hakuna namna ya kuwa-control.
Tanzania isipofanya vema, itaachiwa kizazi cha yatima wa Kitanzania wenye asili ya Burundi
Yangu macho

Upepo Mwanana said...

Nakubaliana nawe Kaka