Monday, March 15, 2010

Hebu Tutafakari Hapa


Kwa wale wanaojua mambo ya kidini...
Hivi kubatiza kwa kumdumbukiza mtu kwenye maji na kumwagia maziwa kichwani na usoni (Kwney picha hii jamaa kalenga jicho la muumini) ni dhehebu gani vile wanafanya hivi.
Kuna yeyote anayejua maana ya kufanya hivi?
Mtanisamehe maana mimi ni mpagani, na mambo ya dini hayajanikaa sana. Huwa najitahidi kusoma biblia angalau huwa naweza kuelewa kilichoandikwa kwani kinasomeka kwa elimu yangu, koran imecharangwa mwandiko nisiouelewa hata chembe!!

4 comments:

Anonymous said...

Wanaofanyia watu hivyo ni kuwapoteza njia watu hao mapadri wasiokuwa na akili ibada inajulikana ni kanisani ama mambo mengine ya uzushi haya ni ya kipumbavu.

chib said...

Heri hayo maziwa wangepelekewa walio na njaa. Kwani sala peke yake haitoshi kukujaza roho wa Mungu, mpaka ushindiliwe maziwa kwenye jicho, Duh!

Halil Mnzava said...

Kitendawili!

Mwacheni MUNGU aitwe --------

Upepo Mwanana said...

Jamani nawashukuru sana kwa kunitembelea hapa