Wednesday, March 3, 2010

Dhana ya kuwatumia Vibaya Watoto


Watoto ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu. Watoto huleta furaha ndani ya nyumba na kwa familia pia.
Watoto wanatakiwa kutunzwa na kufunzwa adabu nzuri mapema ili waje kuwa waadilifu kikazi na kimaisha
Kelele zao huwa kero pale unapokuwa nao, lakini wakiondoka na kubaki mpweke unaweza kutamani kulia :-(
Lakini watu wamekuwa wanawatumia watoto vibaya, kama:
  • Kuwageuza chambo cha kupatia pesa hasa kwa omba omba kuwaanika juani au kuwaweka vifua wazi wakati wa baridi kwenye mitaa ili wapewe kitu kidogo na wapita njia
  • Kuwashindisha njaa ili wakonde na kuwafanya watu wawaonee huruma na kutoa chochote, lakini anayefaidi ni mlezi au muanikaji
  • Kuwageuza marching guys kwa kuwapa bidhaa ndogo ndogo na kwenda kuziuza mitaani, kama vile njugu, karanga na hata mchicha
  • Kuwageuza ngao wakati wa kutokuelewana kati ya wazazi, mwingine anaweza kumtesa mzazi mwenziwe kisaikolojia kwa kumkatalia kumwona mtoto pale wanapotengana, au mwingine kugeuza mashine ya kutengeneza pesa kwa kudai mayumizi ya mtoto wakati anazitumia mwenyewe
  • Wengine wanaanzisha vituo vya watoto yatima lakini kiasi kikubwa cha msaada uingia wanakula wao kwa kujijengea majumba makubwa ya kupangisha, na kila siku kupiga domo la kuomba misaada
  • Wengine wanawatumia kwenye vita, na kuwafundisha kuua
  • Wengine wamewageuza kama sehemu ya kujistarehesha kimapenzi. Kwa hapa natema mate kabisa pwaaaa!
Watoto laiti wangekuwa wanaweza kupata kijarida cha kujieleza... Wangesema mengi.
Labda ndio maana hao hapo kwenye picha wameanza kupoza mawazo mapema kabla shida za dunia hazijawaangukia :-(

No comments: