Monday, November 28, 2011

Hapa Hakuna Soko kwa Madaktari wa Kuremba na Dawa za Kichina

Si kila aliye nayo ni ya asili.  
  
Wafanyabiashara wamegundua au wamebuni makalio ya bandia yanayotengenezwa kiwandani na ya kuyauza kwa akina dada na akina mama wanaotaka kuonekana ya kuwa na wao wamejazia. 
  
Pichani dada wa ..... akijaribu na kupima muonekano wake huku akijiangalia kwenye kioo. 
  
Dunia hii ni ya ajabu, wale walionayo wanatamani yapungue, na wale wasio nayo wanafanya kila juhudi ili wayapate.

Kazi ya Mungu haina Makosa!

4 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Ni vigumu kumuelewa binadamu na mitindo yake ilievamia sasa viungo vya mwili. Mimi naona jamii ilivyohalalisha na kukubali BODY PIERCING ndipo ilikubali yenyewe kuingia bwawani bila kuwa na uwezo wakuogelea huku mashangingi wakike hata wa kiume ndio wao tu bingwa wa mambo ya "kubiasharisha" umbo la mtu hasaa la mtu wakike na sasa sisi tumebaki na kushikwa na butwaa huku tukijiuliza "Je sisi washamba kwakutoyafanya haya ya kunenepesha makalio ya mwanamke, ya kukuuza sehemu za siri kwa wanaume na mambo kama hayo?"!

Anonymous said...

Binadamu kiumbe wa ajabu kabisa. Hii nilikuwa sina habari nayo kabisa!

Yasinta Ngonyani said...

Upepo Mwanana Kwanza za masiku! maana uliadimika kidogo. Hakika binadamu ni halidhiki na alichopewa. Mzungu anataka kuwa mwafrika na mwafrika anataka kuwa mzungu kisa nini jamani????

Upepo Mwanana said...

Ahsante Dada Yasinta. Maisha ndio yananificha hapa na pale.
Ndio hulka ya binadamu, kutokuridhika na jinsi ulivyojaaliwa!!