Tuesday, August 31, 2010

Maadili ya Uchaguzi Tanzania ni Yapi?

Huu ni msimu wa kisiasa Tanzania

Ni vigumu kufunga midomo kuzungumzia siasa hata kama hupendelei mambo ya siasa.


Kuna kitu ambacho sikielewi kuhusu sheria mpya ya matumizi ya fedha katika uchaguzi wa Tanzania, hasa pale wanapozungumzia matumizi ya lugha au kwa kifupi kufuata maadili.


Inaonekana kuna baadhi ya vyama wakihusishwa na tuhuma fulani za ufisadi, hata kama tuhuma hizo hizi zilisababisha watu katika chama hicho kujiuzulu na wengine kushitakiwa, kwa sasa wanakuja juu.


Kwa anaye elewa hayo maadili, naomba anielimishe!!

1 comment:

chib said...

Maadili ni kutokuzungumza ukweli ili watu wasibadili muelekeo wa kuwachagua watu wachafu wanaolindwa kwa sababu mbalimbali